![]() |
| Mtoto wa aliyekuwa gumzo kwa uvutaji sigara akiwa na miaka miwili kinyume cha umri wake, sasa anapenda kula vyakula kwa wingi bila kipimo. |
Mtoto wa aliyekuwa gumzo kwa uvutaji sigara akiwa na miaka miwili
kinyume cha umri wake, sasa anapenda kula vyakula kwa wingi bila kipimo.
Aldi Rizal ambaye kwa sasa ana umri wa miaka mitano alikuwa akijitahidi
kuacha kutumia sigara bila mafanikio na sasa amekuwa na hamu ya kula kila wakati.
Amekuwa akikutwa nyumbani kwao akila vyakula kwa wingi kila mara
kutokana na kupata hamu ya kula kila wakati hali inayomfanya aendelee kuwa
kibonge.
Hivi sasa serikali ya nchi hiyo iko katika mkakati kabambe wa kuzuia
watoto wote kuvuta sigara kwa kuwa ni hatari kwa afya yao pamoja na ya Aldi
pia.
Aliwahi kupelekwa kwa wataalamu jijini Jakarta nchini humo ili apatiwe
tiba ya tatizo lake la kupenda kuvuta fegi kama inavyofahamika.
Alipokuwa huko mama yake alielekezwa kumpatia mwanaye michezo ya watoto
ili asikae bila shughuli hali ambayo ingemtamanisha kuvuta sigara.
Mama yake, Diane Rizal (28) alisema kuna watu bado wanampa sigara
mwanaye lakini anashukuru kuwa anakataa hali inayotia matumaini.
Aldi ambaye kwa sasa ana kilo 25 zaidi ya ule anaopaswa kuwa nao mtoto
wa umri kama wake, mama yake anahofia huenda akaongezeka zaidi.






No comments:
Post a Comment