![]() |
|
Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao
waliofanikisha uzinduzi wa Tovuti Kuu ya serikali.
|
![]() |
|
Waandishi wa habari wakiwajibika. Picha na
Aron Msigwa – MAELEZO.
|
Na.
Aron Msigwa – MAELEZO,Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Mizengo Pinda amesema kuwa kuanzia sasa wananchi wanaweza kupata taarifa na huduma mbalimbali za serikali kwa urahisi zaidi kwa njia ya mtandao katika maeneo wanayoishi bila hata kulazimika kufika kwenye ofisi husika.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali jana (Novemba 29,2013) jioni jijini Dar es salaam, Waziri Pinda amesema kuwa tovuti kuu ya serikali sasa itawawezesha wananchi kupata
taarifa ya huduma mbalimbali za serikali na namna ya kupata huduma hizo kwa
njia ya mtandao na kupunguza usumbufu wa kulazimika kusafiri eneo moja hadi
jingine kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali.
Alisema tovuti hiyo inayopatikana sasa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz ni mojawapo ya juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi, wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi.
Alieleza kuwa tovuti hiyo ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi za Serikali kwa urahisi na kuongeza kuwa licha ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa itawapunguzia Wananchi usumbufu kwa kuokoa muda wa kufuatilia taarifa hizo kutoka eneo moja hadi jingine.
Alisema kuwa taarifa za masuala mbalimbali kuhusu Kilimo, Biashara, Viwanda, Ufugaji, Masoko, Elimu na nyingi zinazohusu taifa la Tanzania sasa zinapatikana kupitia Tovuti Kuu ya Serikali na kutoa wito kwa wananchi kuitumia tovuti hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema kuwa uzinduzi huo umekuja kwa wakati muafaka kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya taarifa mbalimbali za serikali zinazowahusu wananchi katika masuala ya biashara, uwekezaji, kilimo, ufugaji, uhamiaji, nishati na madini na masuala mengine yanayohusu maisha ya kila siku.
Alisema kuwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma itaendelea kufanya kazi bega kwa beg na Wakala ya serikali Mtandao kuhakikisha inaijengea uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kuwahudumia wananchi.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ambao ndio wasimamizi wa tovuti hiyo Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema kuwa Wakala ya serikali anayoisimamia itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa huduma zake kwa wananchi.
Alisema wakala kwa kushirikiana na Wizara, taasisi, mikoa na Halmashauri za
wilaya itaweza kuwahudumia wananchi kwa kuhakikisha kuwa taarifa za serikali
zinapatikana kwa urahisi na kwa kuzingatia muda na kuongeza kuwa italitekeleza
jukumu hilo kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari –MAELEZO ambao ndio wasimamizi wa
maudhui wa tovuti hiyo.
Kuhusu taarifa na huduma zilizomo katika Tovuti Kuu ya serikali Dkt. Jabiri alisema zimegawanywa katika maeneo makuu sita ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje.
Alisema maeneo yote yanalenga kurahisha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.
Alisema tovuti hiyo inayopatikana sasa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz ni mojawapo ya juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi, wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi.
Alieleza kuwa tovuti hiyo ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi za Serikali kwa urahisi na kuongeza kuwa licha ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa itawapunguzia Wananchi usumbufu kwa kuokoa muda wa kufuatilia taarifa hizo kutoka eneo moja hadi jingine.
Alisema kuwa taarifa za masuala mbalimbali kuhusu Kilimo, Biashara, Viwanda, Ufugaji, Masoko, Elimu na nyingi zinazohusu taifa la Tanzania sasa zinapatikana kupitia Tovuti Kuu ya Serikali na kutoa wito kwa wananchi kuitumia tovuti hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema kuwa uzinduzi huo umekuja kwa wakati muafaka kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya taarifa mbalimbali za serikali zinazowahusu wananchi katika masuala ya biashara, uwekezaji, kilimo, ufugaji, uhamiaji, nishati na madini na masuala mengine yanayohusu maisha ya kila siku.
Alisema kuwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma itaendelea kufanya kazi bega kwa beg na Wakala ya serikali Mtandao kuhakikisha inaijengea uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kuwahudumia wananchi.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ambao ndio wasimamizi wa tovuti hiyo Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema kuwa Wakala ya serikali anayoisimamia itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa huduma zake kwa wananchi.
![]() |
|
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifurahia
jambo mara baada ya kuzindua
Tovuti Kuu ya Serikali na kuwataka
wananchi kuitumia katika kupata
taarifa mbalimbali za serikali.
|
Kuhusu taarifa na huduma zilizomo katika Tovuti Kuu ya serikali Dkt. Jabiri alisema zimegawanywa katika maeneo makuu sita ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje.
Alisema maeneo yote yanalenga kurahisha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.
Alisema huduma nyingine katika Tovuti Kuu hiyo
imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje unaopatikana ndani ya tovuti hiyo
ambao unamjengea uwezo mwananchi kufahamu taratibu za upatikanaji wa
huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama upataji wa hati ya
kusafiria, kibali kazi, TIN, cheti cha kuzaliwa na mikopo ya vyuo.
Aliongeza kuwa tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara katika dirisha moja.
Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Tovuti hiyo iliboreshwa na kuunganishwa na
iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz
mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.

No comments:
Post a Comment