Mkongwe wa muziki nchini Congo (DRC) Tabu Ley Rochereau amefairki dunia leo huko Ubelgiji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET

Post Top Ad

Saturday, November 30, 2013

Mkongwe wa muziki nchini Congo (DRC) Tabu Ley Rochereau amefairki dunia leo huko Ubelgiji.

Tabuley, aliyezaliwa November 13, 1940, alikuwa kiongozi wa kundi la Orchestre Afrisa International na mmoja wa wasanii wakubwa katika bara la Afrika katika uimbaji na utunzi wa nyimbo.

Habari zinasema amefariki mapema leo (Novemba 30,2013) asubuhi huko nchini Ubelgiji alikokuwa amelazwa hospitali akiugua kiharusi.

Tabuley, aliyezaliwa November 13, 1940, alikuwa kiongozi wa kundi la Orchestre Afrisa International na mmoja wa wasanii wakubwa katika bara la Afrika katika uimbaji na utunzi wa nyimbo. 

Akiwa na mpiga gitaa hodari Dkt Nico Kasanda, Marehemu Tabu Ley alikuwa mwanzilishi wa mtindo wa Soukous, na kuufanya ukubalike kimataifa kwa kuchanganya midundo ya Cuba na Rhumba la Latin Amerika. 

Tumkumbuke kwa kibao chake "Mokolo Nakokufa"

 Source:Michuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad