CHALENJI CUP 2013/2014:- Zanzibar yaburuzwa 3 huku Kenya ikiitungua Sudani Kusini 3-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 30, 2013

CHALENJI CUP 2013/2014:- Zanzibar yaburuzwa 3 huku Kenya ikiitungua Sudani Kusini 3-1.



Wenyeji  wa CHALENJI CUP 2013/2014, Kenya, leo(Novemba 30,2013) wameifunga South Sudan Bao 3-1 na Ethiopia pia kuichapa Zanzibar Bao 3-1 katika Mechi za Pili za Kundi A zilizochezwa leo huko Nyayo Stadium, Nairobi.
Kwenye Mechi ya Zanzibar na Ethiopia, Bao za Wahabeshi zilifungwa na Fasika Asfan, Dakika ya 5, Salahadin Bargicho, kwa penalti ya Dakika ya 37, na Yonathan Kebede kuingiza Bao la 3 katika Dakika ya 83.

Bao la Zanzibar lilifungwa na Awadh Juma Issa katika Dakika ya 68.

Katika Mechi iliyofuatia, Wenyeji Kenya walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 16 kwa Penati ya Joackins Atudo lakini South Sudan ilisawazisha katika Dakika ya 26 kwa Bao la Richard Jistin.

Katika Dakika ya 29, Jacob Keli aliifungia Kenya Bao la Pili na katika Dakika ya 70, Atudo alikosa kufunga Penati ambayo Kipa wa South Sudan aliokoa lakini Kenya wakapata Bao lao la 3 alilofunga David Owino katika Dakika ya 78.

Ushindi huo unaifanya Harambee Stars ifikishe pointi nne baada ya awali kutoa sare ya bila kufungana na Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi.

Matokeo haya yanamaanisha Kenya na Ethiopia sasa zinalingana kwa kila kitu, pointi nne kila mmoja, mabao matatu ya kufunga na bao moja la kufungwa, wakati Zanzibar sasa ni ya tatu kwa pointi zake tatu na Sudan Kusini inashika mkia.

Jumapili (Desemba 01,2013) zipo Mechi 2 za Kundi B katika ya Kilimanjaro Stars na Somalia na Zambia watacheza na Burundi, Mechi zote zikiwa huko Nairobi Uwanja wa Nyayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad