![]() |
|
Marehemu Dk.
Sengondo Mvungi alipokuwa ICU katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
|
Habari za
kusikitisha zilizotufikia jioni hii(Novemba 12,2013) zinasema kuwa Dk. Sengondo
Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika Kusini alikokuwa
akitibiwa.
Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7 mwaka huu kwa ajili ya
kupewa matibabu zaidi akitokea Hospitali ya Muhimbili kitengo cha MOI ambako
muda wote alikuwa hajitambui baada ya kushambuliwa na majambazi na kuumizwa
vibaya sehemu ya kichwani akiwa nyumbani kwake Kibamba.
![]() |
|
Dakta Sengodo Mvungi
enzi za uhai wake.
|
Wakati Dk. Mvungi
anafariki, jana (Novemba 11,2013) Jeshi la Polisi, kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, lilitangaza kuwakamata watuhumiwa 9 wakiwa na
mapanga yaliyotumika katika uvamizi huo.
Mpaka mauti
yanamfika, Dk. Mvungi alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na
Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB).
Marehemu
aliwahi kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu
wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
MUNGU AILAZE
ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMEEN!







No comments:
Post a Comment