![]() |
Kikundi cha
Mchelemchele kutoka Mwanza kikitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi
wa barabara ya Bwanga – Uyovu inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Geita.
|
Wananchi wa
wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wamenufaika kwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusikilizwa ombi
lao ambapo barabara inayounganisha maeneo ya Masumbwe na Makao Makuu ya wilaya
hiyo imepandishwa daraja na kuwa barabara ya mkoa.
Awali barabara hiyo ilikuwa
ikihudumuwa na wilaya lakini ikipatiwa matengenezo ambayo hayakidhi ongezeko la
magari yanayotumia barabara hiyo kwa sasa.
Aidha Rais Kikwete akiwa njiani kutokea mji wa Masumbwe kupitia makao makuu ya wilaya mpya ya
Mbogwe kabla ya kuingia Geita alisimamishwa mara kadhaa na wananchi wanaoishi
katika vijiji inakopita barabara hiyo ambao walitumia fursa hiyo kuwasilisha
kero zao na hususan suala la barabara ambayo ilielezewa kutokidhi mahitaji
halisi kwa wakazi hao na maeneo jirani.
Akijibu
maombi ya wananchi hao, Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
alielezea kuwa barabara hiyo inayolalamikiwa kwa hivi sasa iko chini ya
usimamizi wa wilaya husika.
Hata hivyo, kwa kuzingatia umuhimu wa barabara
husika na uchanga wa wilaya hiyo mpya, alikipokea kilio cha wananchi hao na
kukubali barabara hiyo ipandishwe daraja
na kuwa ya mkoa.
“Nitatumia
mamlaka niliyopewa chini ya Sheriaya Mfuko wa Barabara Namba 13 ya mwaka
2007 kuipandisha barabara hii ambayo
inaanzia Masumbwe kupitia Mbogwe,
Nyikanga hadi Butengo Lumasa yenye urefu wa kilometa 81 kwamba itakuwa
ya mkoa na hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Tanroads” alisemaWaziri Magufuli.
Aidha,
katika hatua nyingine Mheshimiwa Magufuli
alibainisha kuwa katika mipango ya mwaka ujao wa fedha wa 2014/2015,
wizara yake itaanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara
inayotokea mji wa Katoro hadi Ushirombo yenye urefu wa kilometa 56 ili kuijenga
kwa kiwango cha lami.
Naye Mbunge
wa Mbogwe Bw. Augusto Manyanda Masele kwa upande wake alielezea
kufurahishwa kwake na hatua hiyo na hasa katika kipindi hiki ambacho wilaya
hiyo mpya inahitaji kuimarisha miundombinu mbalimbali kwa lengo la kuharakisha
maendeleo katika eneo hilo.
“Hii imekuwa
ni faraja kubwa kwa wana Mbogwe kwani suala la usafiri limekuwa ni kero ya muda
mrefu, tunashukuru sana kwa kutembelewa na ugeni huu wa Kitaifa hapa mkoa ni
kwetu” alisisitiza Bw. Masele.



.jpg)






No comments:
Post a Comment