![]() |
|
Chelsea drew 2-2 at home with West Brom on Saturday after a 96th-minute Eden
Hazard penalty saved a Premier League point for Jose Mourinho's men at Stamford Bridge.
|
Leo (Novemba
09,2013) wakiwa nyumbani katika uwanja wao Stamford Bridge, Chelsea itabidi
wamshukuru Refa Andre Marriner kwa kuwaokoa toka kwenye kipigo baada ya kuwapa
Penati tata katika Dakika ya 93 wakati West Brom wanaongoza Bao 2-1.
Penati hiyo
ilitolewa na Refa huyo baada ya Mchezaji wa Chelsea Ramires kuanguka baada
kugongana na Steven Reid na Penati hiyo kufungwa na Eden Hazard.
Chelsea ndio
walitangulia kufunga katika Dakika ya 45 kwa Bao la Samuel Eto'o lakini Kipindi
cha Pili West Brom wakafunga Bao mbili kupitia Shane Long Dakika ya 60 na
Stephane Sessegnon Dakika ya 68.
Baada Dakika
90 kwisha Bango likaonyesha Dakika 4 za nyongeza na ndipo Dakika ya 93 ikaja
Penati tata iliyolinda Rekodi ya Jose Mourinho ya kutofungwa Nyumbani kwenye
Ligi.
Nao Wakiwa
kwao Anfield, Liverpool wameifumua Fulham Bao 4-0 kwa Bao za Fernando Amorebieta,
kwa kujifunga mwenyewe, Martin Skrtel na Bao mbili za Luis Suárez.
Ushindi huu
umeifanya Liverpool wakamate Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Arsenal.
LIGI KUU
ENGLAND:-RATIBA/MATOKEO.
Jumamosi
Novemba 9,2013.
Aston Villa
2 Cardiff 0
Chelsea 2
West Brom 2
Crystal
Palace 0 Everton 0
Liverpool 4
Fulham 0
Southampton
4 Hull City 1
LIGI KUU
ENGLAND RATIBA:-Jumapili
Novemba 10,2013.
15:00
Tottenham v Newcastle
17:05
Sunderland v Man City
19:10 Man
United v Arsenal
19:10
Swansea v Stoke







No comments:
Post a Comment