![]() |
| Bi.Dorothy Howe. |
Huko SUSSEX,
Nchini Uinngereza,Bibi Kizee mwenye umri
wa miaka 100 ameibuka na kusema kuwa amevuta sigara laki tano tangu akiwa
msichana mdogo.
Dorothy Howe
ambaye ni katibu muhtasi mstaafu kutoka Uingereza alisema alianza kuvuta sigara
tangu akiwa na umri wa miaka 16 na tabia hiyo ameendelea nayo hadi leo.
Alisema kwa
kuvuta kwake sigara ametumia pauni 193,000 (zaidi ya sh. milioni 400) ambapo
pia hutumia pombe kali aina ya whisky katika maisha yake.
Alipoulizwa
kama ana mpango wa kuacha kuvuta sigara ajuza huyo alisema kuwa hataacha bali
ataendelea na starehe yake hiyo hadi zipande bei.






No comments:
Post a Comment