Wakala wa
Barabara Mkoa wa Mwanza (TANROAD) kutumia kiasi cha shilingi bilioni 1.3
kukamilisha ujenzi wa Daraja la juu kwa watembe kwa miguu eneo la Mabatini Kata
ya Mbugani Wilaya ya Nyamagana Mkoani hapa.
Hatua hiyo
inatokana na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuri kumwaagiza Mkandarasi Kampuni
ya Nordic Consstruction Ltd ambapo garama zote zimetolewa kiasi cha
shilingi milioni 888,530,039/= kwa ujenzi na Mkataba wa Usimamizi
akilipwa kiasi cha shilingi milioni 135,350,000/= na kufanya thamani
kuwa bilioni1.
![]() |
| Waziri wa Ujenzi wa Tanzania John Magufuri. |
Akizungumza
na mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali wa Mkoa ,Wilaya ya Nyamagana, Jiji
la Mwanza jana(Novemba 14,2013) kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi katika eneo la mradi
huo, alisema kwamba Mkandarasi anatakiwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na
kuzingatia Mkataba wake kutokana na kulipwa fedha yote.
Dkt.
Magufuri alisema kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Ujenzi itaendelea
kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa uboresha wa miundombinu
ya barabara na vivuko vya majini na watembea kwa miguu ikiwa ni madaraja.
“Tuliahidi
na sasa tumetekeleza, mnaona leo tumeweka jiwe la msingi na kazi ya ujenzi
inaendelea naamini kufikia Desmba 25 daraja hili litakuwa likifunguliwa na
sherehe za Chrismas watu watapita hapa na kupata frusa ya kupiga picha kama
wanavyofanya kwenye eneo la samaki ikiwa ni kuongeza ajira na utalii”alisema.
“Tumedhamiria
kupunguza msongamano wa magari kuingia mjini na kupunguza vifo ambapo takwimu
za ajari zinaonyesha zaidi ya watu 12 wamekufa na wengine 20 wamepata majelaha
na vilema vya maisha hivyo serikali kuchukua hatua ya kutoa pole kwa
waliopoteza maisha na kuwatakia majeruhi kupona haraka amina” alisema.
![]() |
|
Daraja la
juu kwa watembe
kwa miguu
eneo la Mabatini
Mwanza.
|
Aliongeza
kuwa serikali sikivu ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete itaendelea kuboresha
Miundombinu ambapo hivi sasa Mkandarasi yupo eneo la mradi wa Ujenzi wa
barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17 kwa garama
ya shilingi bilioni 17.9 zilizotolewa na serikali kwa asilimia 100.
“Tumedhamilia
kuondoa msongamano wa magari na watu kulazimika kutumia barabara kufika miji
tayari Wizara yangu tayari imeanzisha mchakato wa kujenga kivuko cha kisasa
ndani ya ziwa Victoria ambacho kitatoa huduma ya usafiri kuanziaia eneo la
Pansiasi kupitia maeneo ya Kirumba mwaloni hadi Nyegezi” alisisitiza
Huku pia
akisisitiza kuweka kwenye mipango ya ukarabati wa ujenzi wa barabara za
Isamilo, Mabatini hadi zahanati ya Kata ya Mbugani na maeneo mengine yaliyosahulika
kwa kuongeza kwenye bajeti ya mwaka ujao kupitia fedha za mfuko wa barabara ili
kuiwezesha halmashauri ya jiji kuzijenga na kuziboresha.
Awali Meneja
wa Tanroad Mkoa wa Mwanza Injinia Leonarld Kadashi akitoa taarifa ya ujenzi wa
mradi huo alisema kuwa Mkandarasi kwa sasa ameisha tekeleza kwa asilimia 60 ya
kazi yake na tayari fidia ya shilingi milioni 9.5 imetolewa kwa uhamishaji
nguzo za Tanesco maeneo yote.
“Ujenzi wa
daraja hili la kisasa unaenda sambamba na upanuzi wa njia tatu badala ya mbili
kwenye barabara ya Nyerere kuanzia eneo la Nata hadi Buzuruga lengo ikiwa ni
kupunguza msongamano wa magari kuingia mjini wakati wa asubuhi na kutoka jioni
kwani mkandarasi yupo eneo la mradi na utatumia bilioni 2 kwa awamu ya
kwanza”alisema na kuongeza.
Kuwa awamu
hiyo ya kwanza itaishia eneo la Sinai na awamu ya pili itaanzia Sinai na
kuishia kwenye daraja la Buzuruga ikiwa ni pamoja na kuweka taa za kuongozea
magari na watembea kwa miguu eneo la makutano ya barabara ya Barnaba na Mahina
kwa garama ya bilioni 2 na kufanya thamani kuwa zaidi ya bilioni 4.
Kwa upande
wake Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula aliomba kwa Waziri Dkt. Magufuri
daraja hilo kuwekewa uzio ili kuzuia watoto kuvuka kiholela hivyo kuhatarisha
maisha yao na kumpongeza kwa juhudi kubwa ya kuendelea kusaidia Jiji la Mwanza
ambapo kiasi cha bilioni 1 alichokitoa kwa jiji hilo kinatekeleza ujenzi wa
barabara za mawe ambazo ni Mkuyuni-Nyakurunduma, Capil point-Idara ya maji,
Sweya-Ihumilo,
Naye Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ametoa ombi maalumu kwa Waziri Magufuri
kuweka mkakati wa kuipanua barabara ya Makongoro inayouelekea Uwanja wa Ndege
toka mjini kati kuwa ya njia nne kutokana na kujengwa jengo la kisasa la kitega
uchumi la Kituo cha Biashara eneo la Ghana na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege
unaoendelea kujengwa kwa sasa kuwa na hadhi ya kimataifa.









No comments:
Post a Comment