![]() |
Padri Joseph
Onesmo Mwang’amba akiwa hospitalini baada ya kumwagiwa tindikali.
|
![]() |
Shehe Fadhil
Suleiman Soraga baada ya kumwagiwa tindikali.
|
![]() |
Padri Ambros
Mkenda akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi.
|
![]() |
Padri
Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi aliyeuawa kwa
kupigwa risasi.
|
![]() |
Kate Gee na
Kristie Trup waliomwagiwa tindikali wakiwa katika matembezi ya kawaida Mtaa wa
Shangani mjini Zanzibar.
|
HAKUNA lugha
nyingine zaidi ya kusema Zenji (Zanzibar) sasa hapakaliki hasa kwa viongozi wa
dini, achilia mbali raia wa kigeni kufuatia kushamiri kwa vitendo vya kuwadhuru
kwa tindikali au silaha, Ijumaa Wikienda lina mfululizo wa mikasa na ifuatayo
ndiyo ripoti kamili.
Ukiachilia mbali mnyororo wa matukio hayo
yaliyosababisha makovu, ulemavu na vifo,
tukio ambalo halijapoa ni la Ijumaa iliyopita ambapo Padri wa Kanisa Katoliki
Parokia ya Machui, Zanzibar, Joseph Onesmo Mwang’amba (60) kumwagiwa tindikali
na watu wasiojulikana.
Tukio hilo
lenye kuunga na mengine nyuma, lilijiri nje ya duka la huduma ya mawasiliano ya
intaneti la Shine Shine lililopo Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi,
Zanzibar ambako padri huyo alikwenda kuperuzi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Afande Haji Hana alikiri kutokea kwa
tukio hilo ambalo lilimfikisha mtumishi huyo wa kiroho kwenye Hospitali ya
Mnazi Mmoja ambako anaendelea na matibabu.
Tindikali hiyo ilimjeruhi padri sehemu za
usoni, kifuani na mkono wa kulia.
Novemba 6,
2012; Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shehe Fadhil Suleiman Soraga alimwagiwa
tindikali na watu wasiojulikana. Alijeruhiwa usoni na mwilini.
Desemba 26,
2012; watu wasiojulikana wamlipiga risasi Padri Ambros Mkenda wa Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Michael, Mpendae mjini Unguja na kumjeruhi vibaya.
Faza Mkenda alipigwa risasi nje ya nyumba
yake. Alikimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Unguja na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Februari
2013; Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi
aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa akiwa kwenye gari akielekea kanisani
kuongoza ibada.
Mei 23, 2013; Sheha wa Tumondo, Mohamed Omar
Said alimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana. Alipata majereha sehemu ya
kifuani na jicho la kulia na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja
mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Agosti 8,
2013; wasichana wawili raia wa Uingereza, Kate Gee (18) na Kristie Trup (18)
walimwagiwa tindikali wakiwa katika matembezi ya kawaida Mtaa wa Shangani mjini
Zanzibar na kujeruhiwa sehemu za uso na kifuani.
Kufuatia
mtiririko huo, habari zinadai kuwa hali ya maisha ya Zanzibar kwa sasa si
shwari kwani viongozi wa kiimani wamekuwa wakitafakari upya jinsi ya kuishi
visiwani humo au kurudi Bara.
Yapo madai
kwamba, baadhi ya viongozi hao wa dini na raia wameingiwa hofu na wamepanga
kuandamana ili kupinga hali ya hatari inayotokana na vitendo hivyo huku kundi
moja lenye imani kali likitajwa kuhusika. Polisi bado inachunguza matukio yote
hayo.
Source:GPL.










No comments:
Post a Comment