Msingi wa maisha
umesimama juu ya hima na kufanya kazi na uzima wa kiroho na kimwili wa mtu na
jamii nao unapatikana kwa kuwa na maisha na uchumi salama.
Kwa msingi
huo katika mkusanyiko salama, wanajamii wote kila mmoja anapaswa kuwa na hisa
yake katika uga wa uzalishaji bidhaa na utoaji huduma na kuwa na nafasi muhimu
katika ushiriki wa masuala ya kijamii.
Kadiri roho
na moyo wa hima na kufanya kazi utakavyokuwa imara na madhubuti katika jamii,
ndivyo ambavyo uwanja wa kuongezeka uzalishaji huandaliwa na matokeo yake kuwa
ni kukua zaidi uchumi jambo ambalo bila shaka lina manufaa makubwa kwa jamii
yoyote ile.
Katika uga
wa mtu binafsi, kuna mlolongo wa mahitaji ya mtu kuanzia chakula na mavazi hadi
kupata daraja katika jamii ambapo mambo haya humsukuma mtu kujituma na kuwa na
bidii katika kufanya kazi ili aweze kukidhi mahitaji yake ya kimaisha.
Katika uga
wa kijamii pia hutokea anga ya ushindani wa wanajamii kwa ajili ya kujipatia
kipato, ushirikiano wa wanajamii na hivyo kukuza roho ya kazi hima na bidii
katika jamii.
Tunashuhudia
leo katika jamii zetu, mtu ambaye hana kazi na ambaye anazurura na kuranda
randa tu mitaani, hana hadhi wala heshima kwa majirani na hata katika jamii
anayoishi.
Lakini mtu
mwenye kazi yake huheshiwa na kuonekana mtu mwenye heshima na hadhi katika
jamii.
Utamaduni na
mafundisho ya vitabu vya mungu vinatoa wito wa kuweko ushirikiano wa pamoja wa
wanajamii na hima za pamoja na yanawataka wanajamii kufanya hima na bidii
katika kazi na kutofikiria maslahi yao binafsi bali kutanguliza mbele maslahi
ya wote.
Natija ya
kuweko mtazamo kama huu huleta roho na moyo wa mfungamano katika jamii.
Ukweli wa
mambo ni kuwa, kila mwanaadamu ananufaika na kustafidi na matunda ya mwenziwe
na hakuna mtu anayeweza kuishi katika jamii bila ya kumtegemea mwenzake hata
kama atakuwa na utajiri wa kutupa; kwani ili aweze kufanyiwa kazi fulani hana
budi kumuajiri mtu.
Hivyo tunaweza kusema kuwa, mtu anapaswa kuwa yuko kwa
ajili ya jamii kabla ya kuwa yuko kwa ajili yake.
Licha ya
kuwa maendeleo ya kiteknolojia yamekuja na kuchukua kwa kiwango kikubwa kazi za
mwanadamu, lakini tunapaswa kusema kuwa, teknolojia yenyewe ni natija ya kazi
na ubunifu wa mwanadamu.
Endapo
mazingira ya kazi hayatoandaliwa basi watu wenye vipaji hawatoweza kuleta
uwanjani uwezo wao na kustafidi na suhula zilizoko kwa ajili ya ustawi na
maendeleo.
Hima na
kufanya kazi ni dhamana ya kubakia na kuongezeka kwa mali na mtaji.








No comments:
Post a Comment