Ndizi ni
matunda yanayopatikana kila mahali. Siku hizi kila penye kioski au grocery ya
matunda ni rahisi kupata ndizi.
Ndizi hizo huuzwa kwa bei ya kawaida tu kwako
kuweza kununua.
Ndizi ni tunda lenye rangi ya kijani liwapo bichi na rangi ya
njano likiwa limeiva vizuri.
Tumezoea kuona ndizi kwenye migomba shambani au
vichane vya ndizi sokoni tunapokwenda kununua vitu mbalimbali kwaajili ya mlo.
Swali ni, je tumeshawahi kujuiliza ni faida gani tunapata tunapokula ndizi
hizo?
Labda huu ni
wakati sahihi sasa tujue manufaa ya kula ndizi mbivu. Na hapa ni baadhi ya
faida za kula tunda hili zuri na lenye lanya tamu.
1. Ndizi
ni tunda lenye vitamin nyingi na madini kadhaa.
-Vitamin
B6 na C hupatikana kwenye ndizi. Vitamin B6 ipo
katika kiwango kikubwa kwenye ndizi ukilinganisha na Vitamin C ambayo ni
kidogo.
Madini yanayopatikana kwenye ndizi ni magnesium, manganese na potassium.
Madini ya magnesium na manganese yana compound inayojulikana kama ‘’cytokinin’’ ambayo
huongeza idadi ya chembe chembe nyeupe za damu hivyo huboresha na kuongeza
kinga ya mwili.
Madini ya potassium nayo husaidia kudhibiti shinikizo kubwa la
damu (high blood pressure) na kuimarisha utendaji kazi wa moyo.
Vile vile
madini ya potassium huzuia upotevu wa madini muhimu ya calcium mwilini ambayo
hutumika katika utengenezaji wa mifupa. Kwa kifupi vitamins na madini
yanayopatikana kwenye ndizi husaidia kupambana na seli za saratani.
2. Ndizi
husaidia kupambana na vidonda vya tumbo.
-Sio tu
kwamba ndizi hupambana na seli za saratani lakini pia hukinga tumbo kupata
vidonda vya tumbo kwa uwezo wa compounds mbalimbali ilizonazo.
Compounds hizi zinazopatikana kwenye ndizi hujenga tabaka nene kwenye kuta za
tumbo ambazo hukinga tumbo kuathirika na tindikali ijulikanayo kama ‘’hydrochloric
acid’’.
Pia ndizi zina enzyme inayojulikana kama ‘’protease
inhibitor’’ ambayo huzuia bakteria wasababishao vidonda vya tumbo.
Huh,…ni faida ilioje. Yani ukila ndizi tu unaweza usimwone daktari kwaajili ya
tatizo la vidonda vya tumbo.
3. Ndizi
huboresha ngozi.
-Kama ilivyo
ngozi yako maganda ya ndizi nayo ni muhimu pia kwani yanaweza kupendezesha
kabisa ngozi yako kama yakisagwa vizuri na matunda mengine kama parachichi.
Virutubisho hivyo kwa pamoja hulainisha ngozi na kuifanya yenye muonekano mzuri
wa kung’aa.
4. Ndizi
huongeza nguvu mwilini.
-Ili uweze
kufanya kazi zako kwa umahiri ni lazima mwili uwe na nguvu. Ndizi mbivu huwa na
sukari ujulikanayo kama ‘’glucose’’ ambayo huongeza nguvu
mwilini. Sukari hii inahitajika katika kiasi maalum mwilini.
5.
Kambakamba za kwenye ndizi husaidia kuimarisha mfumo wa chakula.
-Ni kweli
kabisa kambakamba za kwenye ndizi husaidia chakula kuteleza vizuri kwenye njia
ya chakula. Kwa maana hiyo chakula kinaweza kupita kirahisi bila kipingamizi.
6. Hii labda ndio ulikuwa hujui kabisa ‘’ndizi
husaidia kupunguza stress na kukufanya uwe katika mood nzuri.’’
-Unaweza
kujiuliza kivipi? Kama ulikuwa hujui ndizi zina kemikali mahsusi iitwayo‘’tryptophan’’ ambayo
iwapo mwilini hubadilishwa na kuwa ‘’serotonin’’.
Kemikali hii ya
serotonin iwapo mwilini husaidia mtu ajisikie vizuri na kuwa katika mood nzuri
na hatimaye kupunguza stress. (msongo wa mawazo)






No comments:
Post a Comment