Watu zaidi ya watatu wajeruhiwa vibaya na wengine zaidi ya 50 wanusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Sai - baba Express kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 24, 2013

Watu zaidi ya watatu wajeruhiwa vibaya na wengine zaidi ya 50 wanusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Sai - baba Express kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori.

Askari wa usalama barabarani Iringa wakilitazama basi la kampuni ya Sai - baba Express lenye namba za Usajili T 668 BCD ambalo liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK eneo la Kibwabwa katika barabara kuu ya Mbeya - Iringa jana(Septemba 23,2013) na watu zaidi ya watatu kujeruhiwa vibaya na wengine zaidi ya 50 ambao ni abiria wa basi hilo kunusurika kifo.

Lori la Kampuni ya Ivory lenye namba T 280 ADK lililogongana uso kwa uso na Basi la Sai baba eneo la Kibwabwa katika barabara kuu ya Mbeya - Iringa jana na watu zaidi ya watatu kujeruhiwa vibaya.

Abiria waliokuwa kwenye basi la sai baba. Chanzo:- Francis Godwin

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad