| Muonekano wa Vilima kadhaa ndani ya wilaya ya Ngara ,Biharamulo na hata Karagwe mkoani Kagera vimekuwa na vipara kwa sababu ya uchomaji moto huo pamoja na uharibifu wa Mazingira. |
Katika Vijiji vilivyo pembezoni mwa Barabara kuu ya Rwanda,Burundi hadi Isaka:-Camera ya Mwana wa Makonda Blog ilijionea kilomita kwa kilomita za msitu
ulioteketezwa kwa moto na miti kukatwa.
|
Mabadiliko
ya tabianchi (climate change), uharibifu wa vyanzo vya maji unaofanywa na
wafugaji, na tabia hiyo chafu ya wenyeji ya kuchoma misitu, vinaliangamiza kwa
kasi kikubwa Mazingira yetu.
|
| Japo ni wachache; lakini wakiadhibiwa vikali kama mfano kwa wengine, italeta woga kwa wanavijiji wengine kuendelea na utamaduni huo mchafu unaoteketeza misitu yenye miti mingi. |
Kumekuwa na makabila
makubwa yanayoishi pembezoni mwa Barabara hiyo lakini Si rahisi
kufahamu ni lipi kati ya hayo ambalo limebobea katika tabia hiyo chafu ya
uchomaji misitu.
Katika
kutafuta ni kwa nini hasa wenyeji hupendelea kuchoma misitu wakati wa kiangazi,
Nlipewa majibu tofauti na yenye utata. Kwa mfano, wanavijiji kadhaa, walidai
kwamba baadhi ya wanavijiji huchoma moto misitu ili kuwawinda kirahisi wanyama
wanaokimbia moto japo ukweli hakuna wawindaji.
“Hoja hii
haina uzito wowote, kwa sababu makabila yote yanayopatikana si wawindaji,”shughuli
zao kuu ni kilimo na ufugaji …. Kwa
hiyo, hawezi kuwa wanachoma moto misitu
kwa sababu za uwindaji, kwa kuwa kiasili si shughuli yao.”
Katika
baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, ilitolewa hoja nyingine
kwamba baadhi ya wenyeji huchoma moto misitu wakati wa kiangazi ili mvua
zikinyesha wakati wa masika nyasi nzuri ziote na kwa haraka.
Hoja hiyo
nayo imekuwa ikitumiwa sana na kwa kisingizio cha kuchoma moto ili nyasi nzuri
ziote.
‘’Sababu
nyingine ambayo ilitolewa, na ambayo ina uzito kidogo, ni kwamba uchomaji huo
unafanywa kwa siri na baadhi ya wanavijiji ambao ni wavivu wa kusafisha
mashamba yao kabla ya mvua hazijanyesha’’.
Inaaminika
kwamba moto unawashwa kwa siri na wanavijiji hao katika mashamba yao, lakini
baadaye husambazwa na upepo na kuingilia misitu inayopakana na mashamba hayo na
kuiteketeza.
Hoja hii
inaweza kuwa na mantiki kidogo, lakini kama nilivyoeleza mwanzo, tabia hiyo
chafu inatokana na uvivu na Uduni wa Elimu ya Mazingira.
Je,
Halmashauri za Wilaya Mkoani Kagera na serikali za vijiji, wanafanya nini
kupambana na wanavijiji hao wachache wavivu na wajinga wanaoteketeza misitu kwa moto na Kukata Miti hovyo?
Jibu ni kwamba,
japo sheria ndogo ndogo zimetungwa na kupitishwa katika baadhi ya vijiji
kukabiliana nao; lakini si rahisi kuwakamata kwa kuwa jambo hilo hufanyika kwa
siri mno na msituni.
“Moto
ukiwaka na nyote mkakimbilia huko, bado si rahisi kufahamu nani aliuanzisha. Na
hata kama mtafanya uchunguzi baadaye, itakuwa bado si rahisi kumfahamu
mhusika,” anasema ofisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya NgaraBw.Thoba
Mhina,alipokaririwa Kupitia Mjdala wa asubuhi njema wa Radio Kwizera FM.
Chanzo cha kitendo hicho kiovu ni ujinga, na chanzo cha ‘utamaduni’ huo
hovyo wa kuchoma moto misitu ni ujinga,
na ndiyo maana elimu zaidi kwa wanavijiji hao ndiyo njia pekee ya
kukomesha tabia hiyo.
Lakini pia
ni muhimu sheria ndogo ndogo zinazopitishwa na vijiji na kubarikiwa na
Halmashauri za wilaya, zikatumika kuwaadhibu wale wachache wanaokamatwa, pasi
shaka yoyote, wakichoma moto misitu.
Japo ni
wachache; lakini wakiadhibiwa vikali kama mfano kwa wengine, italeta woga kwa
wanavijiji wengine kuendelea na utamaduni huo mchafu unaoteketeza misitu yenye
miti mingi.





No comments:
Post a Comment