![]() |
|
Watu 61
wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya
waliofariki huenda ikaongezeka. Hata hivyo kuna wengi ambao hawajulikani
waliko.
|
Wananchi wa
Kenya hii leo (Septemba 25,2013) wameanza maombolezo ya siku tatu kama ilivyotangazwa na Rais wa
nchi hiyo Uhuru Kenyatta, maombolezo hayo yanakuja baada ya kutamatika kwa
opersehni nzito ya kuwakabili magaidi walioteka jengo la maduka la Westgate
toka siku ya jumamosi mwishoni mwa juma lililopita.
Kwenye
hotuba yake iliyodumu kwa karibu dakika sitini Rais Kenyatta amevipongeza
vikosi vya Kenya vilivyoshiriki kwenye operseheni hiyo pamoja na ushauri wa
mataifa ya Afrika na Magharibi ambao walishiriki kuhakikisha uasi kwenye jengo
la Westgate unatamatishwa.
Aidha
Kenyatta amewashukuru wananchi wa Kenya kwa ushirikiano waliouonesha toka
mwanzo hadi mwisho wa operesheni yenyewe akieleza kufurahishwa na namna watu
walivyojitokeza kuchangia damu bila kujali eneo wanalotoka wala utaifa wa
wahanga wa tukio la westgate.
Kenyatta
amewahakikishia raia wake ulinzi wa kutosha na kuongeza kuwa taifa hilo ni
salama na wananchi wala wageni wasiwe na hofu.
Katika hatua
nyingine, naibu waziri mkuu wa Somalia ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni
wa taifa hilo, Fawzia Yousouf Haji Adam, amesema nchi yake inawashukuru
wananchi wa Kenya pamoja na wanajeshi wa taifa hilo kwa kufanikisha kurejesha
usalama nchini mwake na kwamba tukio hili linaonesha namna ambavyo Kenya iko
tayari kukabiliana na ugaidi.
Lakini
wakati operesheni hii ikikamilika bado kuna maswali mengi yanayohitaji majibu
kuhusu namna operseheni hiyo ilivyoendeshwa na matukio ya mwisho kwenye
operseheni hii huku kukiwa na hofu kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye
opersheni hiyo huenda ikaongezeka zaidi.
Wakati huo
huo Rais wa Ufaransa, Francois Hollande ametoa wito kwa viongozi wa dunia
kuhakikisha nchi zao zinapambana na makundi ya kigaidi ambayo yameendelea kuwa
kitisho cha usalama wa dunia.
Akiwa mjini
New York Marekani katika mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa Rais Hollande
amegusia tukio la nchini Kenya na kuongeza kuwa ni ishara tosha kuwa makundi ya
kigaidi yanaendelea kupata nguvu na kuua wau wasio na hatia.
Rais Holande
pia amegusia uasi unaoshuhudiwa kaskazini mwa nchi ya Mali na kudai kuwa nchi
yake itahakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha kwa nchi ya mali na nchi
washirika kukabiliana na makundi ya kigaidi.











No comments:
Post a Comment