![]() |
Xiaolian, miaka
22, akiwa na pua mpya ‘iliyopandwa’ na madaktari katika paji lake la uso.
|
Mmoja wa madaktari
walioendesha tiba hiyo akifanya tathmini ya kitaalam kwa Xiaolian.
|
Rai mmoja wa
nchini China anayejulikana kwa jina moja la Xiaolian, mwenye umri wa miaka 22,
ametengenezewa pua nyingine na madaktari ambayo sasa imewekwa kwenye paji lake
la uso, baada ya ile ya asili kuharibika katika ajali ya gari iliyomkumba
Agosti, 2012.
Madaktari
wameitengeneza pua hiyo kwa kutumia sehemu mbalimbali za mwili wa mtu huyo
zikiwemo sehemu za mbavu na ngozi yake.
Operesheni
hiyo imefanyika katika hospitali moja huko Fuzhou, katika Jimbo la Fujian.
Wataalam hao
wanatarajia kuihamisha pua hiyo na kuiweka sehemu ambapo pua yake ya zamani
ilipokuwa.






No comments:
Post a Comment