Shirika la
Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni Unesco, lilitoa
ripoti wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kujua Kusoma na Kuandika Septemba 8 mwaka huu, iliyosema idadi kubwa ya watu hao mbumbumbu wanaishi katika mabara
ya Afrika na Asia.
Pia takwimu
za ripoti zinaonyesha kuwa robo tatu ya wale wasiojua kusoma na kuandika ni
wanawake, na kwamba hali hiyo inaweza kuongezeka hata wakati wa kufikiwa tarehe
ya mwisho ya malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo ni mwaka 2015.
Katika ujumbe
wake kuadhimisha siku hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova alisema kuwa dunia inapaswa kujikagua upya.
Alisema kuwa
dunia ina wajibu wa kuboresha mifumo
yake ya utoaji wa elimu, kwani bila kufanya hivyo kuna uwezekano wa kurudi nyuma kimaendeleo. “ Tunapaswa kumulika
mifumo yetu ya utoaji elimu ili iende sambamba na mahitaji ya wakati” anasema.
Wasiojua
kusoma na kuandika Tanzania.
Ripoti hiyo
ya Unesco imetolewa katika wakati ambapo kiwango cha kujua kusoma na kuandika
nchini kikitajwa kuporomoka.Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002 idadi ya
Watanzania wasiojua kusoma na kundika ilifikia milioni 6.2.
Akizungumza
bungeni, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema
kuwa idadi hiyo ni kwa watu wenye umri
wa miaka 15 na kuendelea, sawa na asilimia 31.
Aliongeza
kusema kuwa kuna uwezekanano idadi hiyo
ikaongezeka kutokana na mazingira yaliyopo sasa.
Alieleza
kuwa watu wasiojua kusoma na kuandika hawajamalizika, na kwamba Sensa ya Watu
na Makazi ya mwaka 2012 bado haikuwa
imetoa mchanganuo wa watu wasiojua
kusoma, kuandika na kuhesabu.
“Ili
kuimarisha Elimu ya Watu Wazima, Serikali inatekeleza mambo mbalimbali, ikiwemo
kuboresha mpango wa awali wa Elimu ya Watu Wazima kupitia programu ya ‘Ndiyo
Naweza’ yenye lengo la kupunguza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika nchini’’
anasema na kuongeza:-
“Serikali
inatumia uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Uwiano Kati ya
Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA), ambapo mpaka mwaka 2012 ulikuwa na
jumla ya wa
Wahitimu
darasa la saba.
Pamoja na
kuwepo kwa mikakati anayotaja Waziri Kawambwa, hali katika ngazi ya elimu ya
msingi haijawa nzuri.
Tafiti zinaonyesha
kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi bila ya kujua kusoma
na kuandika.
Cha kushangaza baadhi ya wanafunzi hao wamekuwa wakichaguliwa
kujiunga na elimu ya sekondari.
Kwa mfano,
Aprili mwaka jana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilibaini kuwepo kwa
wanafunzi wa sekondari 5200 waliokuwa hawajui kusoma na kuandika.
Wanafunzi hao
walikuwa sehemu ya wahitimu wa darasa la saba mwaka 2011.
Awali mwaka
2010, asasi isiyo ya kiraia ya Twaweza ilitoa ripoti ya utafiti iliyobainisha
kuwa kati ya wahitimu watano wa darasa la saba, mmoja hawezi kusoma hadithi ya
kiwango cha darasa la pili.
Utafiti huo
uliopewa jina la ‘Are Our Children Learning’ (Je, watoto wetu wanajifunza),
ulishirikisha sampuli ya watoto 42,033 kutoka kaya 22,800 nchi nzima.
Mikakati ya Nchi.
Tanzania imekuwa ikitekeleza mipango
mbalimbali yenye shabaha ya kuinua kiwango cha watu kujua kusoma na kuandika.
Miongoni mwa mipango hiyo ni ule ulianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1961ambao
unatajwa kuwa ndiyo ulioweka misingi ya hali ya elimu nchini.
Idadi kubwa ya
watu ilijitokeza na kujiunga katika taasisi za mafunzo ya watu wazima.
Mpango mwingine
ulitekelezwa katika kipindi cha mwaka 1964 hadi 1969, na kuweka mkazo wa kuboresha na kuinua elimu ya watu
wazima, au maarufu ‘ngumbaru’ enzi hizo.
Kupitia
mipango hiyo ya uendelezaji wa elimu wa watu wazima, inaelezwa kwamba hadi
kufikia miaka ya 1980, Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi kadhaa duniani ambazo
watu wake wengi walikuwa wanajua kusoma na kuandika.
Kutokana na
hali hiyo, Umoja wa Mataifa uliitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi zilizoko
Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteleleza
mikakati ya kupunguza hali ya kutojua kusoma na kuandika.
Sio kutajwa
tu, Tanzania pia ilipewa tuzo maalumu kwa mafanikio hayo, ambayo watu wengi
wanayanasibisha na dhamira ya dhati aliyokuwa nayo Rais wa awamu ya kwanza,
Mwalimu Julius Nyerere.
Mafanikio
hayo yalichangiwa pia na uanzishwaji wa kampeni iliyoendeshwa katika maeneo ya
vijijini ambako ndiko kulikokuwa na idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na
kuandika .
Nakisomo
907,771.’ Cha kushangaza inaelezwa kwamba kiwango cha kujua kusoma na kuandika
nchini, sasa kimeshuka kutoka asilimia 89.4
mwaka 1986 hadi kufikia asilimia 69
mwaka 2010.
Baadhi ya
wataalamu wa elimu wanasema kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo
kutokana na mwelekeo mpya wa sekta ya elimu.





No comments:
Post a Comment