![]() |
| Boniface Wambura. |
Vitendo
vivyoashiria imani za kishirikina ambavyo vilidaiwa kujitokeza katika mechi ya
Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga, vimeziponza timu
hizo.
Kabla ya
kuanza kwa mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, yaliokotwa mayai katikati ya
uwanja na kisha kukabidhiwa kwa meneja wa uwanja huo, Modestus Mwaluka.
Akizungumza
katika mahojiano maalum na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa
Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema wameshaikabidhi
ripoti ya kamishna na ya waamuzi kwa kamati husika kwa ajili ya kuchukua hatua
zaidi.
"Kwa
sasa sekretarieti ya TFF haiwezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu bado halijapitiwa
na kamati husika. Tumepokea ripoti za waamuzi na kamishna wa mechi na
kuikabidhi kwa kamati husika," alisema Wambura.
"Tukio
hilo liko chini ya TFF kwa sababu ndiyo inayohusika na mambo yote
yanayojitokeza ndani ya uwanja.
"Tusubiri
maamuzi ya kamati husika. Wao ndio wataamua kulingana na kilichomo kwenye
ripoti za maafisa wa TFF waliokuwa wametumwa kusimamia mechi hiyo,"
alisisitiza Wambura huku akikataa kubainisha timu itakayokumbwa na rungu hilo.
![]() |
Meneja wa
Uwanja wa Sokoine Modestus Mwaruka akiwa na mayai matatu yaliyochorwa chorwa
ambayo alidai kuwa ameyakuta katikati ya uwanja.
|
"Klabu
ina wajibu na jukumu la kuhakikisha kuwa wachezaji, viongozi, wanachama na
wapenzi wake wanajiheshimu na hawajihusishi na vitendo vyovyote vya utovu wa
nidhamu kama vile matusi, vitisho, vurugu, vitendo vinavyoashiria imani za
kishirikina na vitendo vyovyote vingine visivyokuwa vya kimichezo,"
inaeleza kanuni hiyo.
Kanuni hiyo
inaendelea kuainisha kuwa: "Klabu ambayo mashabiki wake watafanya vitendo
hivyo, itatozwa faini ya Sh. 500,000 huku shabiki atakayethibitika kujihusisha
na vitendo hivyo, akifungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi kisichopungua miezi
mitatu na kisichozidi mwaka mmoja."
![]() |
Timu ya
Yanga.
|
Agosti 28,
kabla ya kuanza kwa mechi hiyo iliyokuwa ya kwanza kwa Simba kupata ushindi
msimu huu baada ya kushikwa kwa sare ya 2-2 dhidi ya Rhino Rangers mjini
Tabora, ilidaiwa walimwaga maji yenye rangi nyekundu chini ya mlango wa basi
lao wakati wachezaji wao walipokuwa wakishuka kuingia kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo.
"Kamati
inatolea maamuzi mambo ambayo yamo kwenye ripoti za kamishna na marefa tu.
Tukio la ushirikina linalodaiwa kufanywa na Simba jijini Arusha halikuwamo
kwenye ripoti zao. Kamati haiwezi kukaa kuzungumzia suala ambalo halina
ushahidi," alisema Wambura.
Katika hatua
nyingine, TFF imeitupilia mbali rufani iliyowasilishwa na Yanga kuomba kurudiwa
kwa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa madai ya kujitokeza kwa vurugu uwanjani.
Jumapili
uongozi wa Klabu ya Yanga ulisema umewasilisha rufaa TFF kwa njia ya barua pepe
kwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Angetile Osiah kuomba mechi hiyo irudiwe
katika uwanja huru kutokana na vurugu zilizotokea kabla ya mechi hiyo.
"TFF
inashughulikia matukio ambayo yanatokea ndani ya uwanja tu. Vurugu za mashabiki
nje ya uwanja na suala la magari ya Yanga kupigwa mawe ni ya polisi, hatuwezi
kuita kamati kuzungumzia mambo ambayo hayapo.
Source: Nipashe








No comments:
Post a Comment