UEFA CHAMPIONS LIGI:-imeanza kwa kishindo jana Jumanne na Jumla ya mabao 30 yalifungwa katika Mechi 8 za Makundi A hadi D huku Mabingwa Watetezi Bayern Munich wakiichapa CSKA Moscow Bao 3-0 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 18, 2013

UEFA CHAMPIONS LIGI:-imeanza kwa kishindo jana Jumanne na Jumla ya mabao 30 yalifungwa katika Mechi 8 za Makundi A hadi D huku Mabingwa Watetezi Bayern Munich wakiichapa CSKA Moscow Bao 3-0

Cristiano Ronaldo.
Nyota Gareth Bale ametokea benchi na kuipikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake Bernabeu.

Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na kutoa mchango wake kunenepesha ushindi.


Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.

Isco alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.


Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.

Cristiano Ronaldo gestures towards the referee after being brought down

Cristiano Ronaldo hugs Gareth Bale after his second goal of the evening

Isco popped up to open the scoring for Real Madrid, despite the din coming from Galatasaray's fans
Wakicheza kwao Old Trafford, Manchester United wameanza vyema UCL kwa kuichapa Bayer Leverkusen ya Germany Bao 4-2 katika Mechi ambayo wangeweza kufunga Bao nyingi zaidi.

Wayne Rooney
Shujaa wa Mechi hii ni Wayne Rooney alipiga Bao 2 na nyingine kufungwa na Robin van Persie na Valencia.

Bao za Bayer Leverkusen zilifungwa na Simon Rolfes na Omer Toprak.

Bao hizo 2 za Rooney zimemfanya afikishe Jumla ya Mabao 200 kuifungia Man United na sasa yeye yupo Nafasi ya 4 katika Historia ya Klabu hiyo ya kufunga Bao nyingi Listi ambayo inaongozwa na Sir Bobby Charlton mwenye Bao 249.

Back of the net: Rooney's cushioned shot bounces up past Leverkusen keeper Bernd Leno

Robin van Persie (left) leaps to hook in a superb volley to restore United's lead

Consolations: Simon Rolfes (above) and Omer Toprak (below) score for Leverkusen

Rooney celebrates with Chris Smalling and Michael Carrick after his opening goal

All over bar the shouting: Van persie congratulates Valencia after his strike sealed the match
-REAL SOCIEDAD DE FÚTBOL 0 FC SHAKHTAR DONETSK 2

Bao 2 za Kipindi cha Pili za Alex Teixeira zimewapa FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine Ushindi wa 2-0 Ugenini huko Spain walipocheza na Real Sociedad.

KUNDI B

-FC KØBENHAVN 1 JUVENTUS 1

Huko Mjini Copenhagen, FC Kobenhavn na Juventus zilitoka Sare ya Bao 1-1 katika Mechi ambayo FC Kobenhavn walitangulia kufunga katika Dakika ya 14 kwa Bao la Mathias Zanka na Juve kusawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la Fabio Quagliarella.

KUNDI C

-SL BENFICA 2 RSC ANDERLECHT 0

Benfica, wakicheza Nyumbani huko Lisbon, Portugal wameichapa Anderlecht Bao 2-0 kwa Bao za Jurici na Luisao.

-OLYMPIACOS FC 1 PARIS SAINT-GERMAIN FC 4

PSG wameibuka na ushindi wa Ugenini huko Ugiriki walipoichapa Olympiacos Bao 4-1 huku Bao zao zikifungwa na Edinson Cavani, Thiago Motta, Bao 2, na Marquinhos.

Bao pekee la Olympiacos lilifungwa na Weiss.

KUNDI D

-FC BAYERN MÜNCHEN 3 PFC CSKA MOSCOW 0

Mabingwa Watetezi Bayern Munich wameanza vyema kampeni yao ya kutetea Taji lao kwa kuinyuka CSKA Moscow Bao 3-0 kwa Bao za David Alaba, Marijo Mandzukic na Arjen Robben.

-FC VIKTORIA PLZEŇ 0 MANCHESTER CITY 3

Man City wakicheza Ugenini huko Czech Republic wameitwanga Viktoria Plzen Bao   3-0 kwa Bao za Edin Dzeko, Yaya Toure na Sergio Aguero.


MATOKEO:
Jumanne 17 Sep 2013

Manchester United FC 4 Bayer 04 Leverkusen 2

Real Sociedad de Fútbol 0 FC Shakhtar Donetsk 2

Galatasaray A.Åž. 1 Real Madrid CF 6

FC København 1 Juventus 1

SL Benfica 2 RSC Anderlecht 0

Olympiacos FC 1 Paris Saint-Germain 4

FC Bayern München 3 PFC CSKA Moscow 0

FC Viktoria Plzeň 0 Manchester City FC 3

RATIBA:
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu]
Jumatano 18 Sep 2013

FC Schalke 04 v FC Steaua BucureÅŸti

Chelsea FC v FC Basel 1893

Olympique de Marseille v Arsenal FC

SSC Napoli v Borussia Dortmund

FK Austria Wien v FC Porto

Club Atlético de Madrid v Football Club Zenit

AC Milan v Celtic FC

FC Barcelona v AFC Ajax

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad