Wekundu wa
msimbazi Simba SC imeonyesha ni tishio msimu huu baada tya kushinda mabao 6-0
dhidi ya Mgambo JKT katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, huku mshambuliaji Mrundi, Amisi Tambwe akifunga mabao
manne peke yake.
Mabao
mengine ya Simba leo(Septemba 18,2013) yamefungwa na kinda mzalendo, Haroun
Athumani Chanongo, huku wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wakilazimishwa sare ya
1-1 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Matokeo hayo
yanaipandisha kileleni Simba SC baada ya kufikisha pointi 10 kutokana na mechi
nne, huku Yanga SC na Azam FC zinaendelea kusuasua kwa pointi zao sita kila
mmoja baada ya mechi nne.
Tambwe
aliyetokea Vital’O ya Burundi alifunga mabao manne leo katika dakika za nne,
41, 44 na 76 kwa penalti, baada ya beki Bashiru Chanache wa Mgambo kuunawa
mpira kwenye eneo la hatari, wakati Haroun Chanongo alifunga mawili pia dakika
ya 32 na 64.
Kwa ujumla
Simba SC iliwapa raha mashabiki wake leo kwa soka safi na ushindi mnono.
|
Kikosi cha
Coastal Uinion kilichoanza leo.
|
Huko Mbeya;
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Jerry Tegete alitangulia kuifungia Yanga SC
dakika ya 37 akiunganisha krosi maridadi ya winga Simon Msuva kabla ya Michael
Peter kuisawazishia Prisons dakika ya 77 akiunganisha krosi ya Omega Seme
anayecheza kwa mkopo kutoka Jangwani.
Yanga SC
ilicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kupoteza nafasi mbili nzuri za
kufunga mabao zaidi dakika ya tatu, Didier Kavumbangu alipowababatiza mabeki
shuti kali baada ya kupokea krosi ya Simon Msuva na Jerry Tegete dakika ya saba
aliwatoka vizuri mabeki wa Prisons, lakini akapiga nje.
Yanga
walionekana kupigana zaidi kusaka bao la ushindi, lakini Prisons walisimama
imara kuzuia na kushambulia pia na dakika ya 87 almanusra Prisons wapate bao la
pili baada ya Ibrahim Isihaka kupiga kichwa juu kidogo ya lango kufuatia krosi
ya Julius Kwanga.
Kule Uwanja
Chamazi:- Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam,
Kipre Tchetche alitangulia kuifungia Azam dakika ya 21, kabla ya Anthony
Matangalu kuisawazishia Ashanti United dakika ya 79.
Katika
mchezo huo, Azam ilimalioza pungufu baada ya Aggrey Morris kutolewa nje kwa
kadi nyekundu.
Uwanja wa
Mabatini, Mlandizi Mkoani Pwani:- Ruvu Shooting iliichapa 1-0 JKT Ruvu, bao pekee la Cossmas
lewis dakika ya 36.
Uwanja wa
Kaitaba, Bukoba:- Wenyeji Kagera Sugar waliifunga JKT Oljoro 2-1. Mabao ya Kagera yalifungwa na Godfrey Wambura
dakika ya 25 na Maregesi Mwangwa dakika ya 90, wakati la Oljoro lilifungwa na
Shaibu Nayopa dakika ya 35.
Uwanja wa
Manungu, Turiani, Morogoro:- wenyeji Mtibwa Sugar walilazimishwa sare ya bila
kufungana na Mbeya City, wakati Coastal Union ililazimishwa sare ya 1-1 na
Rhino Rangers ya Tabora.
Mkenya Jerry
Santo aliinusuru Coastal kuzama kwa bao la penalti dakika ya 81, kufuatia Salum
Majjid kutangulia kuifungia Rhino dakika ya 26.
RATIBA:
Jumamosi Septemba 21,2013.
Mgambo JKT v Rhino Rangers
Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v JKT Oljoro
Simba v Mbeya City
Azam FC v Yanga
Kagera Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Ruvu Shooting
VPL-MSIMAMO:
|
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
GD |
GF |
POINTI |
|
1 |
Simba SC |
4 |
3 |
1 |
0 |
9 |
11 |
10 |
|
2 |
JKT Ruvu |
4 |
3 |
0 |
1 |
5 |
6 |
9 |
|
3 |
Ruvu Shooting |
4 |
3 |
0 |
1 |
4 |
6 |
9 |
|
4 |
Yanga SC |
4 |
1 |
3 |
0 |
4 |
8 |
6 |
|
5 |
Azam FC |
4 |
1 |
3 |
0 |
2 |
5 |
6 |
|
6 |
Coastal Union |
4 |
1 |
3 |
0 |
2 |
4 |
6 |
|
7 |
Mbeya City |
4 |
1 |
3 |
0 |
1 |
4 |
6 |
|
8 |
Mtibwa Sugar |
4 |
1 |
2 |
1 |
-1 |
3 |
5 |
|
9 |
Kagera Sugar |
4 |
0 |
3 |
1 |
-1 |
2 |
3 |
|
10 |
Rhino Rangers |
4 |
0 |
3 |
1 |
-2 |
4 |
3 |
|
11 |
Mgambo JKT |
4 |
1 |
0 |
3 |
-8 |
1 |
3 |
|
12 |
JKT Oljoro |
4 |
0 |
2 |
2 |
-3 |
2 |
2 |
|
13 |
Prisons FC |
4 |
0 |
2 |
2 |
-6 |
1 |
2 |
|
14 |
Ashanti UTD |
4 |
0 |
1 |
3 |
-6 |
2 |
1 |






No comments:
Post a Comment