|
Wahamiaji wakiwa katika mpaka wa Rusumo Wilayani Ngara
Mkoani Kagera wakiwa katika utayari wa kuvuka
kwenda nchini Rwanda.:-
Picha Na:-Mwanahabari Dullah.
|
|
Maofisa
Uhamiaji, Polisi, Jeshi na Mgambo wakikagua nyumba ya mhamiaji haramu kijijini
Kagarama.
|
|
Vikosi vya
Askari wakiingia kijiji cha Katoro kuanza msako wa wahalifu na wahamiaji haramu
mkoa wa Kager.
|
|
Wahamiaji
raia wa Rwanda wakipata chai hapa ni katika kambi ya Kagemu nje kidogo ya
Manispaa ya Bukobamkoani Kagera.
|
|
Sehemu ya
wahamiaji kutoka vijiji vya Bugabo, Kagabiro-Kasharu, Buhendangabo, Kaagya,
Kishanje Rubafu, Mwizi na Izimbya ndani ya Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.
|
|
Wahamiaji
haramu wakisubiri kurudishwa makwao katika kambi ya Biharamulo mkoani Kagera.
|
|
Watuhumiwa
wa uhamiaji haramu wakiwa katika kambi ya Kagemu nje kidogo ya Manispaa ya
Bukoba mkoani Kagera wakisubiri kuhojiwa.
|
|
Wahamiaji
raia wa Uganda wakisubiri kusafirishwa kwenda mpaka wa Mutukula kurudi makwao.
|
|
Msako
ukiendelea ambapo wahamiaji haramu waliokamatwa katika kijiji cha Kagarama
wakipanda gari ili kupelekwa kambi ya Kagemu kuhojiwa zaid.:-
Picha Na:-Mwanahabari Dullah.
|
Wahamiaji
haramu 194 waliorudishwa makwao wakati wa kutekeleza awamu ya kwanza ya
Operesheni Kimbunga iliyoisha mwishoni mwa wiki iliyopita, wamekataliwa na nchi
zao na kurejeshwa tena nchini.
Mamlaka zinazohusika na operesheni hiyo zimesema
kuwa wamewapokea tena watu hao wakati wanasubiri hatua za kisheria
kuchukuliwa.
Awamu ya
kwanza ya operesheni hiyo ilianza Septemba 6 na kuhitimishwa Septemba 20 mwaka
huu baada ya baadhi ya wahamiaji haramu, kukaidi mwito wa Rais Jakaya Kikwete
wa kurejea makwao na kama wanataka kurudi, wafuate utaratibu wa Sheria.
Taarifa
iliyotolewa na Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Sirro, ilieleza kuwa watu hao
pamoja na kutokuwa na sifa ya kuwa raia wa Tanzania, wamerejeshwa nchini kwa
kuwa pia wamekosa sifa ya kuwa raia wa nchi jirani ambako Serikali iliwapeleka
baada ya vigezo kuthibitisha kuwa ni raia wa nchi hizo.
"Hadi
kufikia mwisho wa Awamu ya Kwanza wa Operesheni hii, timu ya Operesheni
imefanikiwa kukamata wahalifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na
washirika wao na kuhakiki uraia wa watuhumiwa wa uhamiaji haramu," alisema
Sirro.
Kwa mujibu
wa Sirro, kati ya waliokamatwa wapo watuhumiwa 212 wa unyang'anyi wa kutumia
silaha na majangili ambao ni raia wa Tanzania 23.
Silaha
Silaha zilizokamatwa ni mabomu 10 ya kutupwa kwa mkono, silaha 61 zikiwemo
bunduki aina ya SMG (50, Shotgun (8), Mark IV (1), Riffle (1), pistol (1),
pisto za kienyeji (3) na magobori 42 pamoja na mitambo miwili ya kutengeneza
silaha aina ya magobori.
Zingine ni
risasi 665 zikiwemo za bunduki aina ya SMG na SAR risasi 561, shotgun risasi
22, gobori risasi 82 na fataki 8, suruali sare za Jeshi na kibuyu cha maji vya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Sirro aliongeza kuwa wahamiaji haramu
12,704 wamekamatwa, kati yao Wanyarwanda 3,448, Warundi 6,125, Waganda 2,496,
Wakongo 589 Wasomali 44, Myemeni mmoja na raia wa India mmoja.
"Wahamiaji
haramu 2,129 walikubali kuondoka nchini kwa hiari yao; 8,696 waliondoshwa
nchini kwa amri ya Mahakama baada ya kupewa hati ya kufukuzwa nchini na 1,852
waliachiwa huru baada ya Serikali kuthibitisha uraia wao wakati wengine 2,286
wanaendelea na mahojiano ili kuthibitisha uraia wao," alisema.
Kiongozi huyo
wa operesheni alisema ng'ombe 8,226 walikamatwa wakiwa wanachungwa katika
hifadhi za misitu na Sh milioni 32.5 zimepatikana, ikiwa ni tozo za faini ya
ng'ombe walioachwa kwenye hifadhi ya Taifa.
Vingine
vilivyokamatwa ni ngozi za wanyama aina ya duma (1), swala (2), nyati (1) na
vipande 10 vya nyama vinavyodhaniwa kuwa nyara za Serikali.
Vingine
vilivyokamatwa ni vipande viwili vya meno ya tembo pamoja na mbao 2,105, magogo
86, mkaa magunia 467, pombe haramu ya gongo lita 375 na mtambo wa gongo mmoja .
Pia wamekamata bangi kilo 77 na makokoro yanayotumika kuvua samaki kinyume cha
sheria.
"Takwimu
zinaonesha kuwa Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kukamata wahamiaji haramu 7,001,
ukifuatiwa na mkoa wa Kigoma uliokamata wahamiaji haramu 5,005 wakati mkoa wa
Geita wahamiaji haramu waliokamatwa walikuwa 698," alisema Sirro.
Sirro
alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana, kumekuwepo na changamoto
zilizojitokeza, ikiwa ni pamoja na hali ya maisha mchanganyiko ya Watanzania
asilimia 60 na wahamiaji asilimia 40 katika mikoa ya mpakani.
Alitaja
changamoto nyingine kuwa ni baadhi ya wananchi wenye nia mbaya au kulipizana
visasi, waliotaka kutumia operesheni hiyo kukomoana kwa kuwataja baadhi ya watu
kuwa ni wahalifu kumbe ni uongo.
Nyingine ni
baadhi ya wahamiaji baada ya kukamatwa walikosa sifa za uraia wa Tanzania na
hata waliporudishwa kwenye nchi wanazodhaniwa kutoka, walikosa sifa za uraia na
kuleta mgongano kuhusu uraia wao.
Alisema ukosefu wa vitambulisho vya uraia
ulisababisha ugumu wa kutambua wahamiaji haramu.
Pia
kutokuwepo kwa uzio katika mipaka ya nchi yetu, kumesababisha wahamiaji haramu
wanapopelekwa kwao, kurudi kupitia njia za panya. Matarajio Sirro alisema baada
ya kukamilisha Awamu ya Kwanza ya Operesheni Kimbunga, wanatarajia Serikali
itashughulikia changamoto zilizojitokeza, ili kupunguza baadhi ya matatizo
katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita hususan yanayohusu uhalifu na masuala
ya kiuhamiaji.
"Tunatarajia
kuanzisha kikosi kazi kila mkoa, kwa ajili ya ufuatiliaji wa wahalifu sugu
wanaotumia silaha za kivita na wale wanaowafadhili," alisema Sirro.
Alisema
uhamasishaji utafanyika kuanzia ngazi ya familia, kitongoji, mtaa/kijiji, kata,
tarafa, wilaya mkoa na taifa, ili jamii iimarishe misingi ya ulinzi na usalama
kupitia kamati zilizopo na kutoa taarifa mara moja panapojitokeza jambo lolote
linalohusu ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Alisisitiza
kuwa watajipanga kimkakati, ili kuona namna ya kushughulikia baadhi ya
wahamiaji haramu waliokosa sifa za uraia na kurudishwa nchini mwao, ambao
wanang'ang'ania kwa kusema wao ni Watanzania.





No comments:
Post a Comment