![]() |
|
Wenger:
There's even
more to come from Ozil.
|
Ligi kuu
soka nchini Uingereza msimu wa 2013/2014 imeendelea tena leo(Septemba 22,2013)
ambapo katika mchezo wa mapema Arsenal
iliifunga Stoke City Bao 3-1 na kujiimarisha kileleni huku Timu ya Swansea City ikishinda Ugenini.
Mchezaji wa
bei kubwa wa Arsenal,Mesut Ozil alichangia Bao zote 3 walizofunga Arsenal
kwenye Mechi waliyoitwanga Stoke City Bao 3-1 na kuwafanya huo kuwa ni ushindi wao wa 7 mfululizo.
Aaron Ramsey
ndie aliefunga Bao la kwanza na hilo ni Bao lake la 7 katika Mechi 8 kwa
Arsenal.
Stoke
walisawazisha kabla Haftaimu kwa Bao la Geoff Cameron lakini Arsenal wakaongeza
Bao 2 kupitia Per Mertesacker na Bacary Sagna kufuatia frikiki za Mersut Ozil.
Ushindi huu
umewafanya Arsenal wakae kileleni mwa Ligi wakiwa na Pointi 12 kwa Mechi 5
lakini hii leo Tottenham wanaweza kuwapiku Arsenal wakishinda Mechi yao ya
Ugenini dhidi ya Cardiff City.
Nao
Swansea wakicheza Ugenini, walitamba
huku Straika wao Michu akiwa moto na kuitwanga Crystal Palace Bao 2-0.
Michu
alifunga Bao la kwanza baada ya Sekunde 80 tu baada ya kupokea pasi safi kutoka
kwa Jonjo Shelvey.
Michu pia
alichangia kwa Timu yake Swansea kupata Bao la Pili lililofungwa na Nathan
Dyer.
Kipigo hiki
kimewafanya Crystal Palace wabaki kwenye zile Timu 3 za mkiani.
LIGI KUU
ENGLAND RATIBA/MATOKEO:-2013/2014.
![]() |
| Manchester City. |
Jumapili 22
Septemba 2013.
Arsenal 3 –
1 Stoke City
Crystal
Palace 0 – 2 Swansea City
Cardiff City
0 - 1 Tottenham Hotspur
Manchester
City 4 - 1 Manchester United
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||








No comments:
Post a Comment