Malumbano
makali yametokea ndani ya ukumbi wa bunge kwa mara ya pili tangu kuwasilishwa
kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013 kwa kile
kinachodaiwa Muswada huo una mapungufu na haukuwashirikisha ipasavyo wananchi
wa Zanzibar.
Malumbano
hayo yalipeleke Kiongozi wa Kambi rasmi kutolewa nje na Askari wa Bunge baada
ya Muongozo kutoka kambi ya upinzani kumtaka Naibu Spika Kuahirisha Bunge mpaka
Muswada huo utakapofanyiwa marekebisho.
Hali hii
imetokea baada ya hoja kutolewa na mh Ally Seif Mbunge kutoka Chama cha
Wananchi CUF kulitaka Bunge lisitishe Shughuli zake ili Kamati iende Zanzibar
kupata Maoni upya.
Baada ya
muongozo huo Naibu Spika alitoa ufafanuzi lakini Bado hali ikawa tete pale Mh
Tundu Lissu Msemaji Mkuu Wizara sheria na katiba akasimama na kumtupia lawama
wenyekiti wa Kamati ya Kudumu Katiba Sheria na Utawala.
Kwa Mujibu
wa Kanuni za Bunge Viongozi wa Bunge kutoka Serikalini wanaingilia Kati
Malumbano hayo.
Baada ya ufafanuzi
huo wa serikali Bunge linaamua kupiga kura ili Majadiliano ya Muswada huo
Muhimu kwa Watanzania uendelee lakini njia ya kupiga kura haikufua dafu baada
ya Wabunge wa upinzani kuzuia kiongozi wa kambi hiyo asiotolewe nje ya ukumbi
wa bunge.
Hatimaye
Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje na Bunge likaendelea na Mjadala wa
Muswada wa Sheria wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Jumla ya
wabunge wote ni 351, ambao hawakuwepo bungeni ni 136, katika kura zilizopigwa
za ndio ni 59, 156 zimesema sio.
Matokeo hayo
hayakumridhisha kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni Freeman Mbowe ambae
aliomba nafasi ya kuzungumza lakini hakuipata ambapo ndio zengwe lilitokea
mpaka askari kuja kumchukua Mbowe na kumpeleka nje akiambatana na wabunge
wengine wa upinzani.
Awali wakati
wa maswali kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali haiwezi
kuuondoa bungeni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, kutokana na kuzingatiwa kwa hatua zote zinazopaswa kupitiwa wakati wa
maandalizi ya Muswada wa sheria, ikiwemo kuwashirikisha wananchi na wadau
mbalimbali.
Akijibu
swali la Kiongozi ya Kambi ya Upinzani bungeni Freeman Mbowe, wakati wa kipindi
cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Pinda amesema nafasi
iliyopo ni nzuri kwa wabunge wote kuujadili muswada huo, na kubadili vipengele
wasivyoridhika navyo, kabla ya kuupitisha.
![]() |
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
|
![]() |
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi akiteta na Mwanaheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, bungeni
Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
![]() |
Naibu Spika
wa Bunge Job Ndugai akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
kukaa chini, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
|
![]() |
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi
akifafanua jambo Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
|
![]() |
Wabunge wa
Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka
wakae chini , Bungeni Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
![]() |
Wabunge wa
CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5,2013. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
![]() |
Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda akiwa na Bondia Francis Cheka
(katikati) na mkewe Tosha Azenga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma
Septemba 5,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Noma sana ila spika ndo chanzo
ReplyDelete