Matumizi ya baiskeli Afrika-Mzigo wa kilo 300 .. Safari na familia na Hakuna kipato bila baiskeli ..?? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 05, 2013

Matumizi ya baiskeli Afrika-Mzigo wa kilo 300 .. Safari na familia na Hakuna kipato bila baiskeli ..??

Hakuna jambo lisilowezekana - labda hayo yalikuwa mawazo ya bwana huyu kutoka . Amepakia magunia sita ya mkaa kwenye baiskeli yake. 
Mzigo huo una uzito wa karibu kilo 300. Hapo hakuna tena kuendesha, kinachobaki ni kuisukuma baiskeli. Amefunga kamba kwenye usukani ili aweze kuiongoza baiskeli yake vizuri.


Mara nyingi watu wanahitaji muda wa masaa mengi kwenda shuleni au kwenda kuchota maji, kutafuta kuni au chakula. Katika maeneo mengi hakuna usafiri wa umma, magari yanauzwa kwa bei kubwa sana. 
Hivyo wakati mwingine watu wanashindwa kusafirisha bidhaa zao. Lakini mkulima huyu amepata suluhisho. Anaweza kupeleka bidhaa zake sokoni kwa kutumia baiskeli yake.

Mbuzi hawa wamebananishwa kweli! Mmiliki wao anawapeleka katika mnada moja kuwauza. Bila shaka wakishanunuliwa watakwenda kuchinjwa na kuwa kitoweo cha siku husika.

Mtu anayemiliki duka bila kuwa na gari la kusafirishia mizigo lazima atafute mbinu ya kubeba bidhaa mpya kwa ajili ya duka lake. Nchini Tanzania bidhaa hizo hutolewa mijini na kupelekwa sehemu za ndani kabisa vijijini. Waafrika wengi wanapenda kunywa coca cola hivyo muuzaji anayeweza kubeba masanduku mengi ya kinywaji hicho atafaidika.

Katika nchi nyingi za Kiafrika baiskeli hutumiwa kama teksi. Kiti cha nyuma cha kubebea mizigo hutengenezwa vizuri ili abiria aweze kukaa. 
Baskeli hizo zina majina tofauti. Tanzania, Kenya na Uganda zinaitwa "boda boda" au Dala dala, jina linalotokana na maneno ya kiingereza "border to border" - mpaka hadi mpaka. Hii ni kwa sababu katika miaka ya 1960 zilitumika zaidi kwenye maeneo ya mipakani.

Waswahili hunena kwamba-‘’Nguo inapochanika inapelekwa kwa fundi, kiatu kinapoharibika pia kinapelekwa kwa fundi''. 
Mafundi daima wanajua namna ya kusaidia na hata gurudumu linapopata pancha wakati mwingi kuna fundi karibu anayeweza kusaidia. Mara nyingi mafundi wanapatikana kando ya barabara na hivyo wanaweza kutoa msaada wa haraka juu ya kuharibika kwa Baiskeli yako.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad