Taswira ya Malumbano makali yametokea ndani ya ukumbi wa bunge kwa mara ya pili tangu kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 05, 2013

Taswira ya Malumbano makali yametokea ndani ya ukumbi wa bunge kwa mara ya pili tangu kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013.

Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni MhMbowe alitolewa nje ya Bunge leo (Septemba 05,2013) mchana baada ya kukaidi amri ya Naibu spika Mh Ndugai alipomwamuru akae na Mh Mbowe kutotii amri hiyo.


Mh Ngudai aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje, hata hivyo baadaye wabunge karibu wote wa upinzani walitoka pia isipokuwa Mh. Augustin Mrema wa TLP.

Pichani: Mh Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya mjini akitolewa nje bunge.
Malumbano makali yametokea ndani ya ukumbi wa bunge kwa mara ya pili tangu kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013 kwa kile kinachodaiwa Muswada huo una mapungufu na haukuwashirikisha ipasavyo wananchi wa Zanzibar.

Malumbano hayo yalipeleke Kiongozi wa Kambi rasmi kutolewa nje na Askari wa Bunge baada ya Muongozo kutoka kambi ya upinzani kumtaka Naibu Spika Kuahirisha Bunge mpaka Muswada huo utakapofanyiwa marekebisho.

Hali hii imetokea baada ya hoja kutolewa na mh Ally Seif Mbunge kutoka Chama cha Wananchi CUF kulitaka Bunge lisitishe Shughuli zake ili Kamati iende Zanzibar kupata Maoni upya.

Baada ya muongozo huo Naibu Spika alitoa ufafanuzi lakini Bado hali ikawa tete pale Mh Tundu Lissu Msemaji Mkuu Wizara sheria na katiba akasimama na kumtupia lawama wenyekiti wa Kamati ya Kudumu Katiba Sheria na Utawala.

Kwa Mujibu wa Kanuni za Bunge Viongozi wa Bunge kutoka Serikalini wanaingilia Kati Malumbano hayo.

Baada ya ufafanuzi huo wa serikali Bunge linaamua kupiga kura ili Majadiliano ya Muswada huo Muhimu kwa Watanzania uendelee lakini njia ya kupiga kura haikufua dafu baada ya Wabunge wa upinzani kuzuia kiongozi wa kambi hiyo asiotolewe nje ya ukumbi wa bunge.

Hatimaye Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje na Bunge likaendelea na Mjadala wa Muswada wa Sheria wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Jumla ya wabunge wote ni 351, ambao hawakuwepo bungeni ni 136, katika kura zilizopigwa za ndio ni 59, 156 zimesema sio.

Matokeo hayo hayakumridhisha kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni Freeman Mbowe ambae aliomba nafasi ya kuzungumza lakini hakuipata ambapo ndio zengwe lilitokea mpaka askari kuja kumchukua Mbowe na kumpeleka nje akiambatana na wabunge wengine wa upinzani.

Awali wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali haiwezi kuuondoa bungeni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kutokana na kuzingatiwa kwa hatua zote zinazopaswa kupitiwa wakati wa maandalizi ya Muswada wa sheria, ikiwemo kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali.

Akijibu swali la Kiongozi ya Kambi ya Upinzani bungeni Freeman Mbowe, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Pinda amesema nafasi iliyopo ni nzuri kwa wabunge wote kuujadili muswada huo, na kubadili vipengele wasivyoridhika navyo, kabla ya kuupitisha.


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma  Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi akiteta na Mwanaheria  Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kukaa chini, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi  akifafanua jambo Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Bumbumbuli na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5,2013. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini , Bungeni Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya  hivyo na Naibu Spika wa  Bunge, Job Ndugai Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Bondia Francis Cheka  (katikati) na mkewe Tosha Azenga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Septemba 5,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

1 comment:

Post Bottom Ad