Bao la
ushindi kwa Atletico lilifungwa na Mbrazil Diego Costa katika Dakika ya 11.
Ushindi huo
umewafanya Atletico wabaki kileleni wakifungana kwa Pointi na FC Barcelona, ambao
Jana (sEPTEMBA 28,2013) waliifunga Almeria Bao 2-0, na wote sasa wana Pointi 21 kila mmoja baada
Mechi 7 lakini Barca wako juu kwa ubora wa Magoli.
Real
wamebaki Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 5 nyuma.
Katika Mechi
ya Barcelona na Almeria, Lionel Messi aliifungia Barca Bao la kwanza lakini
akalazimika kutoka baada ya kupata matatizo ya Musuli.
Bao la Pili
la Barca lilifungwa na Adriano.
![]() |
Borussia
Dortmund continued their fine start to the
season
with a comfortable 5-0 home
win
over 10-man Freiburg on Saturday.
|
Huko Germany
kwenye Bundesliga, Vinara Borussia Dortmund waliinyuka Freiburg Bao 5-0 na
Mabingwa Watetezi Bayern Munich kuifunga VfL Wolfsburg 1-0.
Bao za
Dortmund zilifungwa na Marco Reus na Robert Lewandowski, Bao 2 kila mmoja na
Jakub Blaszczykowski kupiga Bao la tano.
Kwenye Mechi
ya Bayern Munich, Thomas Muller ndie aliefunga Bao pekee.
Matokeo hayo
yanaifanya Dortmund ikamate usukani ikiwa na Pointi 19 sawa na Bayern Munich
ambao wako Nafasi ya Pili kwa kuzidiwa ubora wa magoli.
RESULTS
Huko Italy
kwenye Serie A. AC Milan na Napoli zote zilishinda kwa AC Milan kuipiga 1-0
Sampdoria kwa Bao la Birsa na Napoli kuichapa Genoa 2-0 Bao zote zikifungwa na
Pandev.
RESULTS
























































No comments:
Post a Comment