Mtoto
Shabani Maulidi akiwa tayari melala kitandani katika hospitali ya wilaya ya
Geita mkoani Geita ....
Habari/Picha Na:- Denice Stephano-Geita.
|
Shabani
akipelekwa wodini na wauguzi kupata matibabu zaidi katika Hospitali ya wilaya ya Geita mkoani Geita.
|
Penye mawe
ni muonekano wa kabuli alilosadikiwa kuzikwa Shaban nyuma ya nyumba yao ambapo mtoto huyo anaelezwa ameonekana akiwa hai.
|
Wadogo zake
na Shabani nao wakiwa wameshikwa na mshangao kama walivyokutwa nyumbani kwao.
|
Mtoto
anayedaiwa kufariki miaka miwili iliyopita
na kufanyiwa matanga ameonekana
akiwa hai Septemba 28,mwaka huu
majira ya mchana baada ya kukutana na mama yake mzazi uso kwa uso wakati akienda kwenye shughuli zake za
kibiashara.
Mtoto huyo Shabani Maulidi (15) alifariki ,alishindwa
kurudi nyumbani kwao tarehe 01.01.2011 wakati alipokuwa amepeleka Mbuzi machungani
kisha kushindwa kurudi nyumbani na baadaye kuonekana baada ya siku tatu akiwa
amefia kwenye kisima cha maji.
Kwa mujibu
wa Baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Maulid Shabani alisema mtoto wake hakurudi
nyumbani siku hiyo,na waliendelea kumtafuta bila mafanikio na ndipo baada ya
siku tatu walimkuta akiwa amefia ndani ya kisima cha maji kilicho maeneo ya
Kijiji cha Nyankumbu Kitongoji cha Mwembeni wilayani Geita.
Baba huyo
alisema baada ya hapo walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kisha waliruhusiwa
kuuchukua mwili wa mtoto wao na kwenda kuuzika nyumbani kwao kitongoji cha 14
Kambarage ndani ya mji wa Geita.
Alisema
walifanya shughuli zote za matanga na wakajua tayari mtoto wao ameishafariki na
kwamba hawakuwa na wazo lolote na kumpata siku zote akiwa hai kama
ilivyotokea akisema ni tukio la
kustaajabisha kwake.
Mama mzazi
wa mtoto
Shabani
menye kilemba
kichwani akiwa amepigwa
bumbuazi
akiwa
maeneo ya hospitali.
|
Mama mzazi
wa mtoto huyo Bi.Aziza Ramadhani akisimulia namna alivyokutana na mtoto wake
alisema alikuwa akienda kwenye shughuli zake za ujasiriamali kama
mfanyabiashara wa mbogamboga akiwa amefika eneo la Nyankumbu nje kidogo sana na
mji wa Geita eneo la Mwembeni alikutana uso kwa uso na mtoto wake.
Alisema
alipomuona alimwita kwa jina lake akisema "mwanagu Shabani ni wewe naye
akamwitikia ni mimi kisha alimshika mkono huku akiwa haamini macho yake ndipo
alipompigia simu mumewe naye akaja wakamchunguza vizuri wakaabaini kuwa ndiye mtoto wao Shabani aliyesadikiwa
kuwa alifariki na kuzikwa.
Akithibitisha
zaidi mama wa mtoto huyo alisema mwanae alikuwa na alama ya kinundu kwenye paji
la uso na mguuni akiwa na alama ya kovu mguuni iliyosababishwa na kuchomwa na
mwiba pia alikuwa na mwanya uliofanana na wa Baba yake mzazi.
Mtoto huyo
aliyevuta hisia za watu wengi mjini
Geita ameendelea kuthibitishwa na walimu wake wa shule ya Msingi Mwatulole
alikokuwa anasoma darasa la tano kabla ya kifo hicho cha utata kwa sasa.
Akiongea na Mwandishi
wa Blog hii, Makamu mkuu wa shule ya msingi Mwatulole Bw.Joseph Nungula
aliyekuwa akifuatilia kwa karibu tukio hilo alisema kweli mtoto huyo anaonekana
ni yeye bila kutia shaka yoyote .
Mwalimu huyo
alisema amemtambua mtoto huyo kwa sura na alama hasa ya usoni huku akimwelezea
mtoto huyo kuwa alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni pia maendeleo yake
kitaaluma yalikuwa mazuri.
Mtoto huyo
ambaye anaendelea kupewa huduma ya kitabibu katika Hospitali ya wilaya ya Geita
kwa uchunguzi zaidi wa kiafya anaongea kwa shida wanapokuwepo watu watu wengi
hata hivyo amemtambua Baba na mama yake mzazi ambapo wanapomuuliza baadhi ya
maswali anawajibu.
Jeshi la
Polisi mkoani Geita ambalo lilikuwa likifuatilia tukio hili kwa ukaribu sana
limethibitisha kutokea kwa tukio hili huku wakiahidi kuendelea kutoa habari
zaidi ambazo tutaendelea kuwajulisha huku Wananchi wakisubiri kibali cha Mahakama
ili kufukua kaburi alililokuwa amezikwa mtoto huyo.





No comments:
Post a Comment