Huu ni mwanzo mzuri kwa Arsenal hasa baada ya Vigogo wengine kupoteza mwelekeo kwa Tottenham na Chelsea kutoka Sare na Manchester United na Manchester City zote kufungwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 29, 2013

Huu ni mwanzo mzuri kwa Arsenal hasa baada ya Vigogo wengine kupoteza mwelekeo kwa Tottenham na Chelsea kutoka Sare na Manchester United na Manchester City zote kufungwa.

Klabu ya Arsenal wamejikita kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza baada ya kuifunga Swansea City Ugenini huko Liberty Stadium Bao 2-1 na wako Pointi 2 mbele ya Timu ya Pili Tottenham.
Baada Mechi 6, Arsenal  sasa wana Pointi 15 na kumfanya Kocha wao  Arsene Wenger afurahie  miaka 17 ya kuwa kazini kama kocha wa Arsenal kwa ushindi wa mabao 2-1 katika Ligi Kuu jana (Septemba 28,2013) dhidi ya Swansea Uwanja wa Liberty.

Shukrani kwao, Aaron Ramsey na kinda Serge Gnabry waliofunga mabao hayo, huo ukiwe ushindi wa 12 mfululizo kwa Gunners katika mashindano yote.

Swansea ilipata bao lake kupitia kwa Ben Davies dakika ya 82, baada ya Gnabry kufunga dakika ya 58 na Ramsey dakika ya 62.

Unaweza sema Huu ni mwanzo mzuri kwa Arsenal hasa baada ya Jana,  Vigogo wengine kupoteza mwelekeo kwa Tottenham na Chelsea kutoka Sare na Manchester United na Manchester  City zote kufungwa.

MATOKEO YA LIGI KUU UINGEREZA 2013/2014.
Jumamosi 28 Septemba,2013.

Tottenham Hotspur 1 Chelsea 1

Aston Villa 3 Manchester City 2

Fulham 1 Cardiff City 2

Hull City 1 West Ham United 0

Manchester United 1 West Bromwich Albion 2

Southampton 2 Crystal Palace 0


Swansea City 1 Arsenal 2

1
ARSENAL FC615
2
TOTTENHAM HOTSPUR FC613
3
CHELSEA FC611
4
SOUTHAMPTON FC611
5
MANCHESTER CITY FC610
6
LIVERPOOL FC510
7
HULL CITY AFC610
8
EVERTON FC59
9
ASTON VILLA FC69
10
WEST BROMWICH ALBION FC68
11
CARDIFF CITY FC68
12
MANCHESTER UNITED FC67
13
SWANSEA CITY AFC67
14
STOKE CITY FC57
15
NEWCASTLE UNITED FC57
16
WEST HAM UNITED FC65
17
NORWICH CITY FC54
18
FULHAM FC64
19
CRYSTAL PALACE FC63
20
SUNDERLAND AFC51

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad