Klabu ya Azam FC imefanikiwa
kufuta uteja kwa Mabingwa wtetezi wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara ,Yanga SC
baada ya leo(Septemba 22,2013) kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Aidha goli la Dakika ya 90 la Mchezaji
kinda aiyepandishwa kutoka kikosi
cha pili,Joseph Kimwaga limewapa ushindi huo Azam FC wa Bao 3-2.
Azam FC
walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya Kwanza tu Mfungaji akiwa John Bocco na Bao hilo kudumu
hadi Mapumziko.
Kipindi cha
Pili Yanga waliibuka na kusawazisha kwa Bao la Kavumbagu na kwenda mbele kwa Bao
2-1 kwa Bao la Hamis Kiiza.
Azam FC
walisawazisha kwa Penati iliyopigwa na Kipre Tchetche baada Kevin Yondani
kushika Mpira na Gemu kuwa 2-2.
Huu unakuwa
ushindi wa pili kwa Azam msimu huu ndani ya mechi tano na sasa inafikisha
pointi tisa, wakati kwa Yanga SC hiki ni kipigo cha kwanza ndani ya mechi tano,
wakiwa pia wametoa sare tatu na kushinda mechi moja, hivyo wanabaki na pointi
zao sita.
Katika mechi
nyingine za ligi hiyo kuu soka Vodacom Tanzania bara, JKT Ruvu ilifungwa 1-0 na
JKT Oljoro Uwanja wa Azam Complex, bao pekee la Paul Malipesa dakika ya 79,
Ruvu Shooting ililala 1-0 mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga, bao pekee la Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 82.
LIGI KUU
VODACOM 2013/2014 MATOKEO.
Jumamosi
Septemba 21,2013.
Mgambo JKT 1
– 1 Rhino Rangers
Tanzania
Prisons 1 – 1 Mtibwa Sugar
Kagera Sugar
3 – 0 Ashanti United
Simba SC 2 – 2 Mbeya City
Jumapili
Septemba 22,2013.
Azam FC 3 -2
Yanga SC
Coastal
Union 1 – 0 Ruvu Shooting
JKT Ruvu 0 –
1 JKT Oljoro
VPL-MSIMAMO:-2013/2014.
| NA | TIMU | P | W | D | L | GD | GF | POINTI |
| 1 | Simba SC | 5 | 3 | 2 | 0 | 9 | 13 | 11 |
| 2 | JKT Ruvu | 5 | 3 | 0 | 2 | 4 | 6 | 9 |
| 3 | Azam FC | 5 | 2 | 3 | 0 | 3 | 8 | 9 |
| 4 | Ruvu Shooting | 5 | 3 | 0 | 2 | 3 | 6 | 9 |
| 5 | Coastal Union | 5 | 2 | 3 | 0 | 3 | 5 | 9 |
| 6 | Kagera Sugar | 5 | 2 | 2 | 1 | 3 | 6 | 8 |
| 7 | Mbeya City | 5 | 1 | 4 | 0 | 1 | 6 | 7 |
| 8 | Yanga SC | 5 | 1 | 3 | 1 | 3 | 10 | 6 |
| 9 | Mtibwa Sugar | 5 | 1 | 3 | 1 | -1 | 4 | 6 |
| 10 | Rhino Rangers | 5 | 0 | 4 | 1 | -2 | 5 | 4 |
| 11 | JKT Oljoro | 5 | 1 | 1 | 3 | -2 | 3 | 4 |
| 12 | Mgambo JKT | 5 | 1 | 1 | 3 | -8 | 2 | 4 |
| 13 | Prisons FC | 5 | 0 | 3 | 2 | -6 | 2 | 3 |
| 14 | Ashanti United | 5 | 0 | 1 | 4 | -9 | 2 | 1 |
**MSIMAMO TOKA TFF






No comments:
Post a Comment