Rais Obama
na mkewe Michelle Obama wakipunga mikono kabla ya kuanza safari ya Kurejea
Washington nchini Marekani.
|
Msafala wa
Rais Obama ukipita maeneo ya buguruni kuelekea uwanja wa ndege.
|
Gari
lililombeba Rais Obama likielekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya
kumaliza ziara yake Nchini Tanzania(Julai 02,2013).
|
Rais wa
Marekani Bw.Barack Obama ameweka mauwa kwenye makaburi ya waathiriwa wa
mashambulizi ya mabomu dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998,
kama ishara ya kuwakumbuka.
Raia 11
wamarekani waliuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na kundi la kigaidi la
al-Qaeda ambaklo lilifanyika wakati mmoja na shambulizi lililofanywa dhidi ya
ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya.
Rais Obama
aliuungana na Rais mstaafu wa Marekani George W Bush kwa kumbukumbu hizo.
Rais Obama alikuwa
na ziara yake barani Africa katika ziara
yake ya pili ya Afrika akiwa Rais , ambapo alitembelea nchi za Senegal , Afrika
Kusini na Tanzania .
Akiwa nchini
Tanzania Rais Obama pia alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaofanywa na
kampuni ya Symbion Power ya Marekani huko Ubungo jijini Dar es Salaam leo(Julai
02,2013).
Tanzania ni
moja ya nchi 9 ambazo zitakazoshirikishwa katika juhudi mpya aliyotangaza Rais
Obama Jumapili (Juni 30,2013) kusaidia
kuongeza nguvu za umeme barani Afrika
hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alitangaza
mpango wa dola bilioni 7 katika hotuba yake katika chuo kikuu cha Cape Town
huko Afrika Kusini na kusema itaongeza uzalishaji wa umeme maradufu kwenye bara
hilo.
Pamoja na
Tanzania juhudi hiyo itaanzishwa Ethiopia , Kenya , Liberia na Nigeria Uganda
na Zimbabwe.
Mradi huo wa
miaka mitano, unatarajiwa kusaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa umeme kusini
mwa jangwa la Sahara,kwa ushirikiano na mataifa ya Kiafrika pamoja na sekta
binafsi.
Akiwa nchini
Tanzania ,Rais Obama pia amezindua
mpango unaonuia kusaidia nchi za Afrika Mashariki ikiwemo, Burundi, Kenya,
Rwanda, Tanzania na Uganda kushirikiana kibiashara.
Wakiwaombea
wahanga hao, mara baada ya kuweka mashada hayo ya maua kwenye mabaki ya vifaa
vilivyolipuliwa na bomu kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment