MCHUNGAJI wa
Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
|
Wananchi
Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical
Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi.
|
Binti
anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi
kwisha.
|
Watoto wa
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba
yao kusomewa kifungo.
|
Mtoto wa
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari
baada ya kesi kumalizika.
|
Waumini
Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika.
|
Watoto wa
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30.
|
Mchungaji wa
Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Lwambi
Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12
baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka
19.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema
Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja
katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema
Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi
Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131
(1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana na
ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na
makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga
mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka
limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande
wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo
kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na
umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa
akiwa na Miaka 57.
Pia alidai
kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo
hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba
mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri
ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo
Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba
kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao
wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha
kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na
viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa
kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa
fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza
kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama
hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
Habari
,Picha na Mbeya yetu Blog
No comments:
Post a Comment