Rais wa
Marekani, Barack Obama na mwenyeji wake, Rais Jakaye Kikwete walionyesha
umahiri wao wa kusakata soka lakini kwa kutumia mpira usiokuwa wa kawaida. |
Rais wa
Marekani Barack Obama akipiga danadana za kichwa alipokuwa katika mitambo ya
kuzalisha umeme ya Symbion Ubungo jijini Dar es Salaam Tanzania.
|
Akipiga
danadana
|
Hebu Nipasie
na mimi uone - Kikwete akisubiri kupasiwa mpira na Obama
|
Rais wa
Marekani, Barack Obama na mwenyeji wake, Rais Jakaye Kikwete walionyesha
umahiri wao wa kusakata soka lakini kwa kutumia mpira usiokuwa wa kawaida.
Viongozi hao
walikuwa kivutio jana kwenye eneo la mtambo wa kufua umeme wa Kampuni ya
Symbion wa Marekani.
Rais Obama
alitembelea mtambo huo ulioko eneo la Ubungo, Dar es Salaam, ambako alitangaza
mpango wa kusambaza umeme kwa nchi mbalimbali za Afrika unaoitwa Power Africa.
Viongozi hao
walionyeshwa mpira huo, ambao uko sawa na ile inayotumika kwenye mechi za soka
lakini unatumika kama chaja ya simu au umeme.
Mpira huo
unaofanya kazi vizuri zaidi baada ya kuchezewa, uligunduliwa na wanafunzi
wawili wa Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani.
Rais Obama
ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua mpira huo na akaurusha juu na kuudaka halafu
akaurusha juu na kuupiga kichwa mara kadhaa.
Baadaye
alitoa pasi kwa Rais Kikwete, ambaye alitoa pasi kwa Obama na kupasiana kwa
muda.
Rais Obama alihoji
bei ya mpira huo na alitaka kujua nguvu ya umeme inayotolewa na mpira ule.
“Kuna chombo
ndani cha kuzalisha umeme. Kadiri mpira huu unavyopigwa ndiyo unatoa nguvu sawa
na betri,” alisema mmoja wa viongozi wa Symbiom wakati akitoa maelezo kwa
Marais Obama na Kikwete.
Hata hivyo,
mpira huo ukichezewa kwa dakika 30 basi unakuwa na nguvu ya kutosha ya kufanya
kazi ya chaja.
Rais Obama
alisema ugawaji wa mipira ni sehemu ya mpango wake wa kusambaza umeme barani
Afrika.
Rais Obama
na mkewe, wakipunga mikono kuwaaga wenyeji wao Rais Jakaya Kikwete na mkewe,
Viongozi wa Kiserikali na wananchi waliofika uwanjani hapo kuwaaga leo, mchana
wakati wakiondoka nchini.
|
Rais Jakaya
Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakipunga mikono kuwaga wageni wao Rais
Obama na mkewe wakati wakiondoka nchini leo mcahana baada ya kumaliza ziara
yao.
|
Source:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment