Watu
takribani bilioni saba duniani hawamjui Mungu wa kweli kutokana na mafundisho
ya kurithi ambayo yanatolewa na viongozi wa dini mbalimbali kwa kutojua usahihi
wa kile wanachowaaminisha waamini wao.
Akizungunza jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya umoja na uelewa wa watu kuhusu
imani ya dini, Nabii Joseph Buberwa idadi hiyo ya watu duniani hawaelewi kweli
Mungu wanayemwabudu na kumtumaini ni yupi.
Alisema
viongozi wa dini zote duniani wanawafundisha waamini wao kuacha maovu na kwamba
watakwenda Mbinguni baada ya maisha ya duniani kitua ambacho si kweli.
Nabii
Buberwa alisema mbali ya kwamba watu hawamjui Mungu wa kweli ambaye jina lake
halisi ni Yehova, bado kuna mambo makuu manne ambayo wameaminishwa kwa makosa
na viongozi wao wa dini.
Aliyataja
mambo hayo kuwa ni kuaminishwa kwamba wanadamu waliokwenda kinyume na matwaka
ya Mungu watachomwa moto milele, maisha ya milele baada ya kifo ni Mbinguni,
watu waliomcha Mungu wote watakwenda Mbinguni na Shetani alikuwa mtawala wa
dunia tangu mwaka wa kwanza wa kuumbwa binadamu.
Alisema fundisho la kwamba watu wakifa kwa kumtumaini
Mungu wataishi milele Mbinguni si kweli na maisha ya milele yako duniani na
kwamba imeandikwa “Mshahara wa dhambi ni mauti” hivyo adhabu ya mtenda dhambi
ni kifo cha milele.
Nabii huyo alisema hawalaumu viongozi wa dini kwa
kufundisha mafundisho hayo ambayo ni potofu kwa kuwa hata wenye hawajui kwamba
wanapotosha na ufafanuzi wa maelezo hayo uko katika kitabu cha Sefania 3:8-9.
Kwa mujibu wa Nabii Buberwa, Mungu amempa mipango ya
kuwezesha vita vikomeshwe duniani ndani ya miaka saba ijayo, kuondoa uhalifu,
ufisadi, umasikini na njaa ndani ya miaka 14 tangu, Novemba 5, 2012.
Alisema watu wanaoamini kwamba baada ya kifo
wakifufuliwa watakwenda Mbinguni na waovu watachomwa milele wanaamini katika
tumaini bandia na hilo limefafanuliwa katika Ufunuo wa Yohana 5:9-10.
Hata hivyo alisema watu 144,000 tu ndio watakaokwenda
Mbinguni kutawala na Yesu Kristo na utawala huo utawahusu Watakatifu
watakaokuwa wako duniani baada ya maisha ya sasa kutoweka na waliokufa
wakitekeleza amri za Mungu watafufuliwa na kujumuika pamoja.
Chanzo:Gazeti la JAMBO LEO.
No comments:
Post a Comment