Nyati wa ajabu anayedaiwa kuwa na rangi ya maziwa huko wa bonde kuu la Ngorongoro (Kreta) na kusababisha tafrani kubwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 09, 2013

Nyati wa ajabu anayedaiwa kuwa na rangi ya maziwa huko wa bonde kuu la Ngorongoro (Kreta) na kusababisha tafrani kubwa.



Nyati wa ajabu.
Wahifadhi  watafiti na wataalamu kadhaa, wako katika harakati za kumsaka Nyati wa ajabu anayedaiwa kuwa na rangi ya maziwa, ambaye hivi karibuni ameonekana katika mwambao wa bonde kuu la Ngorongoro (Kreta) na kusababisha tafrani kubwa.





Kwa mujibu wa mtalaam wa ikolojia katika mamlaka hiyo, Patrice Mattay, uwepo wa nyati (mbogo) huyo wa aina yake hifadhini hapo, kumeibua suala jipya katika utafiti wa wanyama pori, kwani hakujawahi kuwepo Nyati mwenye rangi nyeupe popote duniani. Kwa kawaida Nyati huwa anangozi yenye rangi nyeusi.




Nyati huyo mweupe aligundulika kwa mara ya kwanza na maafisa wa polisi wanaofanya kazi katika kituo cha polisi kilichopo ndani ya hifadhi hiyo, ambao wanasema mnyama huyo hupita katika maeneo ya kituo hicho majira ya asubuhi akiwa miongoni mwa mbogo wengine takribani 20. Ngorongoro ina nyati wapatao 350.


Ni kweli hata mimi binafsi nimemshuhudia Nyati huyo mweupe akikatiza katika sehemu mbalimbali za hifadhi ya Ngorongoro majira ya asubuhi akiwa katika kundi la mbogo wengine,” alisema mkuu wa kituo cha Ngorongoro Afisa wa Polisi, JJ Paul.



Nyati wa ajabu.
Hadi sasa ni maaskari wanaofanya doria katika maeneo ya hifadhi hiyo, hususan nyakati za asubuhi, ndio wanaothibitisha kwa kiwango kikubwa kumuona Nyati huyo wa ajabu ambaye sasa anatarajiwa kuwa atakuwa kivutio kipya cha utalii nchini.



Meneja Uhifadhi katika mamlaka ya Ngorongoro, Amiyo T. Amiyo amesema tayari shirika lake limekwisha tuma askari wake kadhaa kumsaka Nyati huyo wa ajabu, ili kubaini eneo ambalo anapatikana kwa ajili ya kuwezesha utafiti zaidi.



“Na kwa mtu yeyote mwenye kutuletea taarifa kuhusu Nyati huyo mweupe zitakazotuwezesha kumpata mnyama huyo, basi naye pia atazawadiwa ipasavyo,” alisema Amiyo.



Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ndiyo inayoongoza kwa kupata watalii wengi nchini na kwa mujibu wa Ofisa Utalii wa Shirika hilo, Asantaeli Melita, zaidi ya wageni 585,000 hutembelea eneo hilo, na hasa Kreta, kila mwaka.



Idadi ya wanyamapori walioko Ngorongoro kwa sasa inafikia 300,000 wengi wao wakiwa ndani ya bonde lenyewe huku baadhi na hasa twiga wakiishi nje ya Kreta.



Mbali na Mbogo wa jabu aliyegunduliwa hivi karibuni, eneo la Ngorongoro pia lina maajabu mengine kadhaa, ukiwemo kilima cha mchanga unaotembea bila kusambaratika, idadi kubwa ya Kakakuona, mnyama anayedaiwa kuwa na uwezo wa kutabiri, pamoja na idadi kubwa ya wanyama adimu kama Mbwa-mwitu na Faru.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad