|
Mkimbiza
Mwenge wa uhuru Kitaifa mwaka huu 2013,Bw.Seperatus Lubinga akikata mkungu wa Ndizi wakati wa Mbio za
Mwenge huo (Julai 07,2013) wilayani Ngara mkoani Kagera
baada ya yeye na wenzake kupewa zawadi kutoka kwa Mkulima wa migomba
wilayani humo na Kuzindua miradi 11 yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 1 na Milioni 973,641,404.
|
|
Wakimbiza
Mwenge wa uhuru Kitaifa wakifurahia ndizi mbivu baada ya kujikatia mkungu
shambani walipopewa zawadi na Mkulima wa ndizi Kata ya Kabanga wakati wa Mbio za Mwenge huo (Julai 07,2013) wilayani
Ngara mkoani Kagera .
|
|
Hapa
ni Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Ngara mkoani Kagera Bw.Kostantine kanyasu(Mrefu mwenye kofia nyeupe kichwani)
wakati wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru(Julai 07,2013) eneo la Benako wilayani
Humo.
|
|
Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Bw.Deogratius Ntukamazina(mwenye suti) akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ,wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Ngara mkoani Kagera Bw.Kostantine kanyasu(Mrefu mwenye kofia nyeupe kichwani)
wakati wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru(Julai 07,2013) eneo la Benako wilayani
Humo.
|
|
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2013 akiwa mwenge huo baadhi ya Madiwani ambapo katikati ni Diwani wa Viti Maalumu CCM tarafa ya Kanazi Niniani Bakari na Kulia kwake ni Kaimu mwenyekiti wa halmashauri na diwani wa Kata ya murusagamba Bw.Sudi mkubira
wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru(Julai 07,2013) wilayani Ngara mkoani Kagera.
|
|
Hapa
ni baadhi ya Wananchi wakionekana juu ya mti kufatilia kinacho endelea katika eneo la Mkesha wa Mwenge Kata ya Kabanga
wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru(Julai 07,2013) wilayani ngara mkoani Kagera.
|
|
Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu 2013 kama ishara ya Ukarimu kwa wakimbizaji hao kutoka kwa Wananchi na Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
|
|
Wananchi hapa wakiserebuka katika sherehe za Mkesha wa mwenge ,ulipokesha katika Kata ya Kabanga Wilaya ya
Ngara mkoani Kagera .
|
Ukiwa wilayani Ngara Mkoani Kagera Mwenge wa Uhuru
ulikagua pamoja na Kuzindua Miradi 11 mbalimbali
Katika sekta ya Elimu ya Msingi,Mifugo na Uvuvi,Hifadhi ya
Mazingira,Maendeleo ya Jamii,Sekta ya Utawala na Vijana yenye thamani ya
Shilingi Bilioni Moja na Milioni 973, 641,404.
Aidha Mwenge wa Uhuru ulimaliza mbio zake wilayani
Ngara (Julai 08,2013) Asubuhi na Kukabidhiwa wilayani Biharamulo mkoani Kagera ambapo ukiwa wilayani humo utakagua na kuzindua miradi 10 mbalimbali ya Kimaendeleo yenye thamani ya
zaidi ya shilingi Bilioni 2.
Kauli mbiu ya Mwaka huu katika Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru ni''Watanzania ni wamoja''Tusigawanywe kwa Misingi ya tofauti zetu za Dini,Itikadi,rangi na Rasilimali''
|
Viongozi
mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani
Kagera Bw.Kostantine kanyasu(Mrefu mwenye kofia nyeupe kichwani) wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru(Julai 07,2013) wilayani ngara mkoani Kagera.
|
|
Baadhi ya Wananchi wa wilaya ya Ngara Mkaoni kagera waliojitokeza ,wakifatilia kinachoendelea katika mbio
za Mwenge wa Uhuru(Julai 07,2013) wilayani humo.
|
|
Hapo ni Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu
2013 wakikata mkungu wa Ndizi ikiwa ni Zawadi waliyopewa na Mkulima mmoja wa
kata ya Kabanga wilayani Ngara
ambapo ulipokuwa wilayani Ngara Mwenge wa Uhuru ulikagua pamoja na Kuzindua Miradi 11 yenye
thamani ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni 973, 641,404.
|
No comments:
Post a Comment