|
Hiki
ndicho Kikosi cha Timu ya Chivu FC kilichoifunga Timu ya Kigina FC magoli 3-1
siku ya Jumapili ya (Juni 30,2013) katika uwanja wa shule ya Msingi Chivu,kata ya
Ntobeye wilayani Ngara mkoani Kagera ,na Kubeba Kombe lenye thamani ya shilingi elfu 50 kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya
Ayubu Meshaki Kabaka maarufu Mtesa CUP 2013.
|
|
Hiki
ndicho Kikosi cha Timu ya Kiginau FC kilichofungwa na Timu ya Chivu FC magoli 3-1
siku ya Jumapili ya (Juni 30,2013) katika uwanja wa shule ya Msingi Chivu,kata ya
Ntobeye wilayani Ngara mkoani Kagera ,na Chivu FC Kubeba Kombe lenye thamani ya shilingi elfu 50 kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya
Ayubu Meshaki Kabaka maarufu Mtesa CUP 2013.
|
|
Timu zote Chivu FC na Kigina FC zikiwa uwanjani
siku ya Jumapili ya (Juni 30,2013) katika uwanja wa shule ya Msingi Chivu,kata ya
Ntobeye wilayani Ngara mkoani Kagera , kucheza mchezo wao wa fainali kuwania Kombe lenye thamani ya shilingi elfu 50 kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya
Ayubu Meshaki Kabaka maarufu Mtesa CUP 2013.
|
|
Mgeni
rasimi katika fainali hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP 2013 kata ya Ntobeye – Mdau Mkubwa wa Michezo hapa
wilayani Ngara na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM- Issa
Samma akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Chivu FC kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
|
|
Mgeni
rasimi katika fainali hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP 2013 kata ya Ntobeye – Mdau Mkubwa wa Michezo hapa
wilayani Ngara na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM- Issa
Samma akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Kigina FC kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano hayo. |
|
Kulia
Mwenye shati la Kijani ni Muandaaji wa
Mashindano hayo,Katibu wa Vijana Kata ya
Ntobeye-UVCCM Ayoub Kabaka Mtesa na Kushoto
ni Afisa mtendaji wa kata ya Ntobeye Sprian Senyamba wakiwa Uwanjani kusalimiana na wachezaji wa timu zote.
|
|
Mashabiki
kutoka Vijiji vya Kata ya Ntobeye wakifatilia mchezo wa Fainali hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP 2013 kati ya Kigina FC dhidi ya Chivu FC
ilichezeshwa na Mwamuzi Jofrei Bizimana ,ambapo Kigina FC walifungwa
bao 3-1 na Chivu FC.
|
|
Kushoto ni Afisa mtendaji wa kata ya Ntobeye Sprian Senyamba ,Mgeni
rasimi katika fainali hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP kata ya Ntobeye kwa mwaka huu –Mdau Mkubwa
wa Michezo hapa wilayani Ngara na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa ya Chama cha
Mapinduzi CCM-Issa Samma (mwenye shati jeupe) akiwa na Muandaaji wa Fainali hizo Katibu
wa Vijana Kata ya Ntobeye- Ayoub Kabaka Mtesa (shati la Kijani) wakifatilia
Fainali ya mashindano hayo Kati ya Chivu FC dhidi ya Kigina FC katika uwanja wa
shule ya Msingi Chivu ambapo Kigina FC walifungwa bao 3-1.
|
|
Huyu ni Kipa wa Chivu FC katika mchezo huo alikutwa na kamera ya Mwana wa Makonda Blog akiidakia Timu yake bila ya kuwa na Viatu wala Jezi katika mchezo huo wa Fainali ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP 2013 kati ya Kigina FC dhidi ya Chivu FC
ilichezeshwa na Mwamuzi Jofrei Bizimana ,ambapo Kigina FC walifungwa
bao 3-1 na Chivu FC.
|
|
Mashabiki
kutoka Vijiji vya Kata ya Ntobeye wakifatilia mchezo wa Fainali hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP 2013 kati ya Kigina FC dhidi ya Chivu FC
ilichezeshwa na Mwamuzi Jofrei Bizimana ,ambapo Kigina FC walifungwa
bao 3-1 na Chivu FC.
|
|
Mgeni
rasimi katika fainali hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP kata ya Ntobeye kwa mwaka huu –Mdau Mkubwa
wa Michezo hapa wilayani Ngara na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa ya Chama cha
Mapinduzi CCM-Issa Samma (mwenye shati jeupe) akiwa na Muandaaji wa Fainali hizo Katibu
wa Vijana Kata ya Ntobeye- Ayoub Kabaka Mtesa (shati la Kijani) wakifatilia
Fainali ya mashindano hayo Kati ya Chivu FC dhidi ya Kigina FC katika uwanja wa
shule ya Msingi Chivu ambapo Kigina FC walifungwa bao 3-1.
|
|
Aliyeshika Mic ni Mzee Juma Niokindi Ndalirengeje akiwa ni Mzee mwanzilishi wa Kijiji cha Chivu akiongea mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali na Kumpa Issa Samma mwenye shati jeupe jina la CHAKUTUMAINI kutokana na jitihada zake mbalimbali za kuinua na kuendeleza Michezo wilayani Ngara mkoani Kagera.
|
|
Mashabiki
kutoka Vijiji vya Kata ya Ntobeye wakifatilia utoaji wa zawadi kwa washindi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP 2013 kati ya Kigina FC dhidi ya Chivu FC
ilichezeshwa na Mwamuzi Jofrei Bizimana ,ambapo Kigina FC walifungwa
bao 3-1 na Chivu FC kuwa Mabingwa wa kombe hilo kwa mwaka huu.
|
Jumapili
ya (Juni 30,2013) katika uwanja wa shule
ya Msingi Chivu,kata ya Ntobeye wilayani Ngara mkoani Kagera ,wenyeji Chivu FC
waliutumia vyema uwanja wao na kuibuka na Kombe lenye thamani ya shilingi elfu
50 kwenye mchezo wake wa fainali wa
mashindano ya Ayubu Meshaki Kabaka
maarufu Mtesa CUP .
Huku
wakishangiliwa mno na Mashabiki wao ,Chivu FC walishuka katika mchezo huo wa fainali wakiwa na hamasa hiyo dhidi
ya wenzao Timu ya Kigina FC na
kufanikiwa kuwafunga magoli 3-1.
Magoli
hayo ya Chivu FC yalifungwa na Nelsoni Amoni magoli mawili moja likiwa kwa njia
ya penati kipindi cha kwanza cha mchezo huo ,huku goli la tatu likifungwa na
mchezaji Abubakari Jumaa.
Aidha
bao la kufutia machozi la Kigina FC lilifungwa na mchezaji wao Mateso
Richardi kwa penati kipindi cha pili na kumfanya Nahodha wa timu hiyo Mussa
Jemedari mpira ulipomalizika kukubali
matokeo hayo ya kufungwa bao 3-1 na Chivu FC huku akisema beki yao ndio
imewaangusha .
Fainali
hiyo ya Ayubu Meshaki Kabaka Mtesa CUP
kati ya Kigina FC dhidi ya Chivu FC ilichezeshwa na Mwamuzi Jofrei Bizimana na kuwafanya wachezaji wote wa timu mbili
zilizokutana kusifia maamuzi ya refali
huyo huku Nahodha wa Mabingwa wa
kombe hilo Chivu FC- Felix Feniasi licha
ya kushinda amesema mchezo ulikua mzuri ,wenye nidhamu na wakuburudisha
mashabiki waliojitokeza kuushuhudia.
Mshindi
wa kwanza katika fainali hiyo ambaye ni
Chivu FC aliondoka na zawadi ya fedha taslimu shilingi elfu 30 huku mshindi wa
Pili Kigina FC akiondoka na zawadi ya shilingi Elfu 20.
Lakini mgeni rasimi katika fainali hiyo ya Ayubu Meshaki
Kabaka Mtesa CUP kata ya Ntobeye kwa
mwaka huu –Mdau Mkubwa wa Michezo hapa wilayani Ngara na Mjumbe wa Halmashauri
kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM-Issa Samma licha ya kuongezea zawadi kwa
washindi ya shilingi elfu 50 kwa kila timu ,aliipongeza Kamati ya Kombe hilo kuandaa mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya Wanamichezo 80 wa soka kutoka timu 6 zilizoshiriki kutoka kata ya Ntobeye
na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano hayo.
Aidha
akisoma Risala ,Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano kwa niaba ya kamati ya
Mashindano hayo Ibrahimu Mpita alisema
kuwa timu zilizoshiriki zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za vifaa vya
michezo ambavyo ni pamoja na Mipira,Jezi,Nyavu za kwenye magori,Vibendera vya
Waamuzi,Timu shiriki kukosa Walezi na Mikopo ya Vijana haitolewi kwa Vijana hao
ili waweze kumudu Maisha yao.
Akijibu
risala hiyo Mgeni rasim –Issa Samma alisema yeye ni Mlezi wa timu zote
zilizopo hapa wilayani Ngara na kwamba
kadili ya uwezo wake atahakikisha changamoto zilizopo za kimichezo
anazitatua pamoja na kushirikiana na
Viongozi wenye nia ya dhati kuendeleza michezo ili kuhamasisha na kukuza
michezo wilayani Ngara mkoani kagera.
Aidha
alisema kwa kushirikiana na Viongozi wenye nia ya dhati kuleta Maendeleo ya
Michezo,yuko tayari wakati wowote atakapofuatwa na Viongozi hao kutoa Vifaa
vyake Vya Ujenzi ili kukarabati Viwanja ambavyo vitakuwa vinahitaji marekebisho
ikiwa ni Pamoja na Kiwanja cha Michezo cha Shule ya Msingi Chivu ambacho hivi
karibuni kinatarajiwa kuanza kufanyiwa ukarabati.
Pia
aliwataka Vijana hao kujiunga katika Vikundi ili iwe rahisi kwao kupata fursa
ya kupatiwa Mikopo .
Kwa
Upande wake Muandaaji wa Mashindano
hayo,Katibu wa Vijana Kata ya
Ntobeye-UVCCM Ayoub Kabaka Mtesa alisema kuwa Lengo la kuwa na Fainali hiyo
ni kuleta changamoto kwa Vijana wa kata
ya Ntobeye ili waweze kuiva Kimichezo badala ya kujiunga na Makundi ya Wavuta
bangi na mambo mengine machafu.
Pia
alisema kuwa anaishukuru Kamati ya Mashindano ya Fainali ya Ayubu Meshaki
Kabaka Mtesa CUP kwa kusimamia vema
Mashindano hayo na kumalizika bila kuwa na vurugu huku yakileta faida kwa
wachezaji kwa afya zao na kuwakutanisha
pamoja wana Ntobeye.
No comments:
Post a Comment