Poulsen na Juma Kaseja. |
Poulsen
akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho kinachojiandaa
na michuano ya CHAN na kiporo cha mechi
ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Gambia, amesema amekuwa akisoma na kusoma
sana habari zinamhusu Kaseja na klabu yake kupitia kwenye vyombo vya habari,
lakini yeye kwa upande wake amesema bado anamuamini Kaseja na ataendelea kuwa
mchezaji muhimu ndani ya kikosi chake:
"Nimekuwa
nikisikia taarifa nyingi zinamhusu nahodha wetu Juma Kaseja, ningependa kuweka
suala hili wazi kwamba Kaseja bado ni mchezaji mzuri na anafanya kazi nzuri
sana ndani ya timu ya taifa.
Juma Kaseja. |
Ni nahodha
mzuri kwa sababu ni kiongozi mzuri kwa wenzie nje na ndani ya uwanja.
Hivyo kwangu
hali itaendelea kuwa vile vile na nategemea kesho kumuona akijiunga na kambi ya
timu ya taifa, ataendelea kuwa nahodha na pia golikipa namba 1 wa kikosi
changu. Kuhusu yeye na klabu yake nisingependa kuyaingilia, lakini kwangu
Kaseja bado ni muhimu kwa sababu amekuwa akifanya nzuri kwenye timu ya taifa.
Kuhusu hatma ya huko mbele, tusubiri muda utaongea," alisema Kim Poulsen.
Wachezaji
wengine walioitwa kwenye timu ya Taifa ni kama ifuatavyo: Makipa - Juma Kaseja
Ally Mustapha, Mwadini Ally, Aishi Mwanula.
Mabeki:
Aggrey Morris, Kevin Yondani, Canavaro, Shoamari Kapombe, Erasto, Vicent, David
Luhende.
Viungo: Mcha
Khamis, Kazimoto, Sure Boy, Domayo, Chanongo, Kiemba
Washambuliaji:
Mrisho Ngassa, Simon Msuva, John Bocco, Juma.
No comments:
Post a Comment