Huu ndio Ujumbe wa leo Kutoka klabu ya Soka ya Bodaboda FC ya Ngara Mjini ,wilayani Ngara Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 05, 2013

Huu ndio Ujumbe wa leo Kutoka klabu ya Soka ya Bodaboda FC ya Ngara Mjini ,wilayani Ngara Mkoani Kagera.


Klabu hii ya Soka ya Bodaboda FC ya Ngara Mjini ,wilayani Ngara Mkoani Kagera imeanzishwa hivi karibuni na Wajasirimali/Waendesha Pikipiki aka Bodaboda/Sekido  waliojiajiri ili kupata kipato cha kumudu maisha yao ya Kila siku.



Aidha Uongozi wa klabu hiyo ya Bodaboda FC uko katika kutekeleza mikakati ya kuijenga  timu yao ili iwe moja kati ya Timu zitakazoleta upinzani wa kisoka katika mashindano mbalimbali ya Michezo yatakayokuja siku za usoni.



Hapa wanaonekana Wanachama,Wapenzi na Mashabiki wa Bodaboda FC wakijianda na safari yao ya  kwenda kucheza michezo mbalimbali ya kirafiki na Vilabu vya Jirani vya wilaya ya Ngara mkoani Kagera,Lengo ikiwa ni pamoja na kuitangaza timu yao,Kujifua kimazoezi na Kudumisha Upendo na Ushirikiano.



Maneno hayo:-''Ukishukuru,Utazidishiwa.......''pia unaambiwa..''Ni afadhari  Kuchakaa Nguo kuliko Akili.....''.



Hapa wanaonekana baadhi ya Wachezaji na Viongozi wa Bodaboda FC kwenye picha ya Pamoja katika uwanja wa Kijiji cha lemela wilayani Ngara mkoani Kagera  tayari kucheza mchezo wao wa kirafiki na wenyeji wao Lemela FC ,Lengo ikiwa ni pamoja na kuitangaza timu yao,Kujifua kimazoezi na Kudumisha Upendo na Ushirikiano.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad