|
Kikosi cha
wabunge wapenzi wa Simba katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,tayari kwa
mchezo wao uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga jana (Julai 07,2013).
|
Kikosi cha
wabunge wapenzi wa Yanga pamoja na waamuzi wa pambano lao dhidi ya Simba katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 , uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga jana (Julai 07,2013).
|
Historia
imeandikwa! Jana Jumapili, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ulitingishika
kutokana na burudani ya nguvu iliyotolewa kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini
2013, lililoanza mapema asubuhi na kurindima hadi usiku mnene, Timu ya Ijumaa
Wikienda ilikuwepo mwanzo mwisho.
JK NDANI.
Tamasha hilo
la kila mwaka ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, lilianza mishale ya asubuhi na baadaye
burudani ya muziki wa dansi ilichukua nafasi wakati umati mkubwa wa watu ukianza
kuingia uwanjani hapo.
UFUNGUZI.
Bendi ya
Mlimani Park ‘Sikinde’ ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufungua pazia la burudani na
kufuatiwa na Msondo, waliowakosha vilivyo mashabiki waliokuwepo huku Romani
Mng’ande ‘Romario’ akigeuka kivutio kikubwa kwa jinsi alivyokuwa ‘anayarudi’
jukwaani.
Baada ya
burudani tamu ya muziki wa dansi kutoka kwa Sikinde na Msondo, waimbaji wa
Injili nao walianza kulishambulia jukwaa kwa zamu.
Waimba
Injili, Edison na Ambwene Mwasongwe, waliwajibika ipasavyo jukwaani na
kushangiliwa sana, baada ya hapo, Mwenyekiti wa Taasisi ya East Africa Speakers
Bureau (EASB), Paul Mashauri alitoa neno la matumaini na ujasiriamali.
INJILI.
Baada ya
hapo, ‘maemsii’, Steve Mengere ‘Nyerere’ na Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ waliruhusu
mlipuko wa muziki wa Injili uendelee, waimba Injili wa Tanzania na Kenya wakawa
wanapishana jukwaani wakiwemo Martha Mwaipaja, Enock, 24 Elders na Sarah K
kutoka Kenya, Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, Solomon Mukubwa,
Glorious Singers na wengine kibao, asikwambie mtu upako ulishuka!
JK.
Baada ya
burudani hiyo, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo alihutubia kisha
kumkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara aliyemkaribisha Rais Kikwete.
Katika
hotuba yake, Rais Kikwete aliwahimiza
Watanzania kutokubali kubaguliwa kwa itikadi za kisiasa na kidini na kuwasihi
kuendeleza mshikamano.
DIMBANI.
Baada ya
kumaliza kuhutubia, Kikwete alishuka dimbani na kuwakagua wachezaji wa timu za
wabunge wa Simba na Yanga kisha akapuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa mechi
hiyo.
JK AFUNIKA.
Rais JK
alifunika ile mbaya baada ya kuchukua kipyenga na kukipuliza kwa umaridadi
mkubwa kuashiria kuanza kwa mchezo, hali iliyowafanya wengi kuamini kweli ni
mdau wa michezo aliyekamilika.
Wimbo ya
Taifa ukipigwa, kila mtu mguu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika
uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013).
|
JK
akisalimiana na wachezaji wabunge wa Simba katika Tamasha la Usiku wa Matumaini
2013 ,lililofanyika uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013).
|
JK
akisalimiana na wachezaji wabunge wa Yanga katika Tamasha la Usiku wa Matumaini
2013 ,lililofanyika uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013).
|
Bango likiwa na Maelezo wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
SOKA SAFI
UWANJANI.
Wabunge wa
Simba na Yanga walioneshana soka dimbani lakini mpaka mwamuzi wa mchezo huo,
Othman Kazi anapuliza kipyenga cha mwisho, si Simba wala Yanga waliokuwa
wameliona lango la mwenziye hivyo kuamuru mshindi apatikane kwa changamoto za
penalti.
Wabunge wakikwaana uwanjani. |
NI YANGA
KATIKA USIKU WA MATUMAINI 2013.
Baada ya
kupigiana penalti, Timu ya Yanga iliibuka kidedea kwa kuilaza Simba kwa jumla
ya penalti 4 kwa 3 hivyo kombe maalum lililoandaliwa likanyakuliwa na Timu ya
Wabunge wa Yanga na kukabidhiwa kwao na Waziri Mukangara.
SOKA BONGO MOVIES v/s BONGO FLEVA.
Wakati
shamrashamra za ushindi zikiendelea, Timu za Bongo Movie na Bongo Fleva nazo
zilijitupa uwanjani.
Katika mechi
hiyo, Bongo Fleva ndiyo waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za wenzao lakini
baada ya muda, Bongo Movie walichomoa kupitia kwa mshambuliaji wao, Vincent
Kigosi ‘Ray’ na kufanya ubao wa matangazo usomeke 1-1.
Mpaka
mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho, bado matokeo yalikuwa ni sare, hali
iliyolazimu ipigwe mikwaju ya penalti ambapo Bongo Fleva waliibuka na ushindi
wa penalti 2-1.
MZEE YUSUF.
Mzee Yusuf
na kundi lake zima la Jahazi Modern Taarab, walivamia steji na kuwakosha
vilivyo maelfu ya mashabiki waliohudhuria.
KITUKO.
Wakati Mzee
Yusuf akikandamiza stejini, jamaa mmoja ambaye jina halikupatikana alijikuta
akigeuka kituko baada ya kupandwa midadi na kuvua nguo hadharani.
NDONDI /
MASUMBWI.
Baada ya
kumalizika kwa mechi hizo kisha Mzee Yusuf kutumbuiza, uliwadia wasaa wa masumbwi
ambapo Mbunge wa Viti Maalum (UV-CCM), Ester Bulaya alifungua ulingo kwa
kuzichapa na Aunt Ezekiel na matokeo ya jumla, wote wawili walifungana pointi
katika pambano hilo la raundi mbili.
Baada ya
hapo, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alifuana na Jacqueline Wolper na
matokeo yalikuwa ni wawili hao kufungana kwa pointi hivyo hakukuwa na mbabe.
Katika
Tamasha la Matumaini 2013, Jackline Wolper na Halima Mdee walizipiga
....hapakupatikana mshindi baada ya kutoka Droo.
|
Pambano hilo
lilipomalizika, Vincent Kigosi ‘Ray’ alipanda ulingoni akiwa tayari kuzichapa
na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe lakini kutokana na sababu
zilizokuwa nje ya uwezo, mheshimiwa huyo hakutokea ulingoni hivyo Ray kuibuka
na ushindi wa mezani.
MIYEYUSHO,
MASHALI WAWAKALISHA WAKENYA.
Ilifika zamu
ya mapambano ya kimataifa ambapo Francis Miyeyusho wa Tanzania alipanda
ulingoni na Shadrack Muchanje kutoka Kenya.
Katika
pambano hilo la kuvutia, Miyeyusho alimshikisha adabu mpinzani wake raundi ya
kwanza katika dakika ya pili na kumtoa kwa Knock-Out (KO).
Baada ya
kuibuka na ushindi huo, Miyeyusho alikabidhiwa Ngao ya Amani ya Afrika Mashariki
na Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally.
MASHALI
AMKALISHA MKENYA.
Pambano la
mwisho la raundi sita, lilikuwa ni kati ya Mkenya Patrick Amote aliyerushiana
mawe ya ukweli na Mtanzania Thomas Mashali.
Licha ya
ukali wa Mashali, Mkenya Amote aliweza kustahimili mno lakini mwisho katika
raundi ya sita, Mashali alimkalisha Amote kwa KO na kufanya ngao ya pili ya
Amani ibaki Bongo.
MUZIKI.
Uwanja wa
burudani ya muziki ulifunguliwa na msanii chipukizi, Ommy aliyelianzisha na
wimbo wake mpya wa My Number One.
Baada ya
hapo, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ alipanda stejini na kuamsha shangwe za nguvu
kutokana na umahiri mkubwa aliouonesha wa kukata mauno sambamba na wacheza shoo
wake.
WANAUME
FAMILY.
TMK Wanaume
Family walipopanda jukwaani baada ya H. Baba kumaliza, uwanja mzima ulilipuka
kwa shangwe za kufa mtu.
Chegge na
Temba walifanya makamuzi ya nguvu kwa nyimbo kali kama Nampenda Yeye, Dar Mpaka
Moro na nyingine kibao huku wakionesha uwezo mkubwa wa kuyarudi mapanga shaa!
PREZOO,
DIAMOND WEE ACHA TU.
Baada ya TMK
Wanaume Family, mkali kutoka 254, Nairobi nchini Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’
alikwea jukwaani kwa staili ya aina yake, jukwaa likawaka moto wakati mchizi
alipowakilisha nchi yake.
Prezzo akiwa kwa steji na Nelly Kamwelu. |
Cash Money
Brother huyo akiwa amechafuka na mikufu kibao ya dhahabu aliendelea kumwaga
makamuzi ya nguvu huku uwanja mzima ukimshangilia kwa nguvu.
DIAMOND
STEJINI.
Mgenge
Prezzo alipomaliza Shoo kali, Rais wa Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alijitupa
jukwaani kwa mbwembwe za hali ya juu akiwa sambamba na wacheza shoo wake na
kusababisha watu washindwe kukaa kwenye viti vyao, kila mmoja akawa anajiachia
kivyake na swaga za Platnumz.
Ngoma kali
kama Ukimwona, Nimpende Nani... ziliwabamba kinomanoma maelfu ya watu waliokuwa
wamefurika uwanjani.
HISTORIA
IMEANDIKWA!
Watu wa kada
mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na wanasiasa walikiri kuwa tamasha
hilo limeandika historia ambayo haijawahi kutokea, jambo ambalo hata JK
alilikiri.
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara akimkaribisha JK kutoa hotuba yake katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika
uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
Mwandaaji wa
tamasha Eric Shigongo akiongea machache katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika
uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
JK akiongea
na kadamnasi wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
JK akipungia
umati unaomshangilia kwa nguvu wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika
uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
Mashabiki
wakiwa nje ya uwanja wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika
uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
Mshabiki wa
Yanga akielekea uwanjani katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 ,lililofanyika
uwanja wa Taifa jana (Julai 07,2013) .
|
Habari Na:
Timu ya Ijumaa Wikienda.
No comments:
Post a Comment