![]() |
|
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwasili katika mkutano huo kwa helkopta.
|
![]() |
| Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani. |
Watu wawili
wanahofiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa kutokana na
mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa Chadema katika eneo la Soweto,
kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa Mkutano wa Chadema wa kumaliza
kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana (Juni 15,2013) .
Bomu hilo
lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho
Taifa,Bw. Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika
Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
| Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko. |
Hilo ni
tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, kwani Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua
watu watatu na wengine kujeruhiwa.
Habari
kutoka eneo la tukio zimedai kwamba mlipuko huo ulitokea karibu na gari la
matangazo la Chadema aina ya Mitsubishi Fusso lililokuwa jirani na jukwaa
alilokuwa akilitumia Mwenyekiti wa Chama hicho,Bw. Freeman Mbowe jana jioni.
Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti amesema katika hospitali yake kuna
maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.
Habari
zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu
wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao
haijafahamika.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amesema katika
tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi
ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali
mbalimbali mkoani humo.
Taarifa
zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la
jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa
akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza
kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto
hali iliyozidisha taharuki.
Baada ya
tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa
maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako
jukwaani.
Hali hiyo
ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.
Hali hiyo ya
watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti
watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha
taharuki.
Baadhi ya
watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na
wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine
waliokuwa katika eneo hilo.
![]() |
| Wafuasi wa Chadema. |
Jana(Juni
15,2013) Chadema ilikuwa ikifunga
kampeni zake eneo hilo kusubiri uchaguzi mdogo wa udiwani ambazo zinafanyika
sehemu mbalimbali nchini sambamba na uchaguzi mdogo wa ubunge Chambani, Pemba,
Zanzibar.
Sambamba na
Chadema pia vyama vya CUF na CCM vilifunga kampeni katika eneo hilo moja,
wakati CUF iliyohutubiwa na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba ikifanyika
stendi ya mabasi ya Kampala Coach, huku CCM ikihutubiwa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye ilifunga kampeni zake katika kituo cha mabasi yaendayo
Sanawari.
Mei 5,2013 takribani watu watatu walikufa katika Kanisa
hilo nje kidogo ya Mji wa Arusha, na wengine kadhaa walijeruhiwa huku Balozi wa
Vatican nchini na watawa waliokuwa katika shughuli maalumu ya kuzindua Parokia
mpya ya Mtakatifu Yosefu walinusurika.
Aidha Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali
Hassan Mwinyi amesema mantiki ya demokrasia ya vyama vingi si kujenga chuki,
uhasama na ugomvi bali ni shime ya ushindani wa nguvu ya hoja itokanayo na
ushawishi wa kisera bila umwagaji damu na mfarakano.
Alhaji
Mwinyi alitoa kauli hiyo jana, wakati akifunga kampeni za CCM katika mkutano wa
hadhara katika Kijiji cha Mapape, Mkoa wa Kusini Pemba.
Kata 26
nchini leo(Juni 16,2013) zinafanya
uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na madiwani kwa sababu mbalimbali.
TAARIFA
KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA JANA,Juni 15,2013.















No comments:
Post a Comment