![]() |
|
Ndege
ya shirika la EasyJet.
|
Shirika
la ndege, linalotoa huduma za usafiri wa ndege kwa bei nafuu Fastjet, limepata
kibali cha kuanzisha safari za ndege za kimataifa za bei nafuu, kutoka Tanzania
hadi Afrika Kusini, Zambia na Rwanda.
Kampuni
hiyo inayomilikiwa na Stelios Haji-Ioannou, ambaye ni mmiliki wa shirika la
ndege la Easyjet, lililo na makao yake barani ulaya.
Shirika
hilo limetangaza kuwa litaanzisha safari za ndege katika mataifa hayo kwa bei
nafuu huku abiria wakilipa dola mia moja pekee.
Kwa
sasa shirika hilo linahudumia wasafiri nchini Tanzania pekee.
Raia
wengi na hasa wafanya biashara wamefurahishwa na tangazo hilo, wakisema kuwa
itapunguza gharama za usafiri na hivyo kuimarisha biashara katika kanda hiyo.
Nchini
Kenya, shirika la ndege la Kenya Airways ambalo ni moja ya mashirika makubwa ya
ndege barani Afrika, limepata pigo kubwa baada ya kupata hasara kubwa katika
kipindi cha miaka minne iliyopita.
Ripoti
zinasema kuwa shirika hilo lilipata hasara ya zaidi ya dola milioni mia moja
kabla ya kutozwa ushuru, kiwango ambacho ndicho mbaya zaidi tangu mwaka wa
2009.
Shirika
hilo lilikuwa maarufu sana kwa abiria wanaosafiri magharibi, mashariki, kusini
na katika mataifa ya Afrika ya kati.
Chanzo:BBC.






No comments:
Post a Comment