![]() |
Rosemary Peter. |
Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary Peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.
Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.
![]() |
Rosemary
peter akipongezwa baada ya kuvishwa Taji la Redd’s Miss Nyamagana 2013,baada ya
Mshindi wa Taji hilo Diana Amimo kudanganya Uraia na Umri wake.
|
![]() |
Rosemary
peter hapa anavishwa Taji la Redd’s Miss Nyamagana 2013,baada ya
Mshindi wa Taji hilo Diana Amimo kudanganya Uraia na Umri wake.
|
![]() |
Rosemary
peter mshindi Taji la Redd’s Miss Nyamagana 2013,baada ya
Mshindi wa Taji hilo Diana Amimo kudanganya Uraia na Umri wake.
|
Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14.
Aidha Sindano la kumtafuta Mrembo wa mkoa wa
Mwanza linatarajiwa kufanyika June
14,2013 katika viwanja vya Yatch Club jijini Mwanza.
Warembo 18
kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamejitokeza kushiriki shindano hilo
la aina yake huku....Burudani inayosubiriwa kwa hamu kubwa ni Mh. Mbunge Joseph
Mbilinyi maarufu kama sugu atakapo panda jukwaani kukumbushia enzi
hizo...akishindikizwa na mkali mwingine wa Chege Chigunda kutoka TMK.
Warembo wote wanatarajiwa kuanza kabi rasmi Jumanne hii katika moja ya hoteli maarufu jijini humo.
Itakumbukwa mkoa wa Mwanza tayari ulishatoa Mrembo wa Tanzania, ambaye ni Nasreem Karim 2009 na Miriam Gerald 2010.
Pamoja na
mchakato wa shindano la urembo kuendelea kwa hivi sasa nchini, macho na masikio
yapo mkoani Mwanza, ambako kumekua kukileta changamoto na upinzani mkali wa
warembo kila Mwaka.
Picha na :
Mukhsin
Mambo.
No comments:
Post a Comment