|
Hapa ndipo
eneo ambalo Daladala iliingia wakati ilijaribu kulipita Gari lingine ikiwa Mwendo
kasi na kuukutana na Tela la Mafuta.
|
Daladala hiyo
kwa Upande wa nyuma yenye namba za
usajili T 635 ALS ikiwa imeharibika vibaya Baada ya Ajali kutokea Eneo la Ifisi
Mbalizi Mkoani Mbeya(Juni 06,2013).
|
Lori aina ya Scania yenye namba ZA usajili T378 AGD likiwa limepaki Baada ya ajali hiyo kutokea. |
Juu na Chini
ni Wananchi mbalimbali wakiwa wanashuhudia Mabaki ya daladala baada ajali hiyo iliyo tokea Ifisi Mbalizi Mkoani Mbeya(Juni 6,2013).
|
Watu
17 wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuharibika vibaya
kufuatia ajali iliyohusisha Gari la abiria aina ya Toyota Hiace na Scania.
Ajali hiyo
imetokea leo majira ya Saa Saba Mchana katika eneo la Ifisi nje ya Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Ifisi(ICC) Mbeya Vijijini.
Mashuhuda
wa ajali hiyo wamesema gari la abiria Toyota Hiace lenye namba za usajili
T 635 ALS likiendeshwa na Nikutusya Mwanja likitokea Mbalizi kuelekea Songwe
iliingia kwenye Trela la Scania lililokuwa likitokea Tunduma kuelekea Dar Es
Salaam.
Wamesema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari ndogo ambapo Dereva alikuwa
akijaribu kulipita gari lingine lakini mbele akakutana na Lori ambalo
alipojaribu kulikwepa akaingia kwenye Trela lake na kupinduka vibaya.
Trela hilo
lenye namba za usajili T 675 ACT likiwa linavutwa na Kichwa chenye namba za
usajili T 378 AGD halikuweza kuumia sana kutokana na kwenda kwa mwendo mdogo
ambapo majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitale teule ya Ifisi kwa matibabu
zaidi.
Muuguzi Msaidizi
wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimath Sanga amethibitisha kupokelewa kwa majeruhi
17 na kwamba kati ya majeruhi hao 3 hali zao siyo nzuri sana ingawa majina yao
hayakuweza kupatikana.
Ameongeza
kuwa majeruhi wengi wameumia sehemu za kichwani na miguuni na kwamba baada ya
kumaliza kupatiwa huduma ya kwanza wataangalia ni wangapi wanaweza kuruhusiwa
na wengine kulazwa.
Hata hivyo
habari kutoka eneo la tukio zimesema kuwa Kondakta wa gari dogo aliyefahamika
kwa jina moja la Ayubu alitoweka mara baada ya kutokea kwa ajali ingawa
haifahamiki kama ni kurukwa kwa akili au ni kukimbia kesi.
No comments:
Post a Comment