Facing
history: President Obama took a tour of Goree Island outside of Dakar, Senegal
where slaves used to be depart on boats bound for America in the late 18th
century
|
President
Obama was accompanied to Goree Island by his wife Michelle, their eldest
daughter Malia, Michelle's mother Marian Robinson and their niece Leslie
|
The Obamas
visited Goree Island's Door of No Return where the slaves would embark on their
journeys across the Atlantic Ocean
|
Obama peered
out at the crashing waves through the island's 'Door of No Return,' at first by
him
|
Mrs Obama
joined him at the poignant doorway, and he said that the visit helped remind
them of the importance of protecting civil rights
|
Ulinzi
katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais
yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.
|
Rais wa Marekani
Barack Obama amewasili nchini Afrika kusini leo(Juni 28,2013) kuendelea na ziara yake ya nchi
tatu katika bara la Afrika inayolenga kupanua uhusiano wa Marekani na bara
hilo.
Ziara yake
imekuja wakati kukiwa na wasiwasi wa afya ya kiongozi aliyepigania haki dhidi
ya ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela, ambaye yupo mahututi katika hospitali ya
Pretoria.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliopanda ndege ya Rais ya Air Force One, Ijumaa bwana
Obama alisema sio lazima kwake
kumtembelea bwana Mandela katika hali yake ya sasa.
Maafisa wa
White House walisema Alhamis kuwa ziara ya aina hiyo wanaiachia jukumu familia
ya Mandela. Jumamosi (Juni 29,2013) Rais Obama anapanga
kutembelea kisiwa cha Robben, gereza ambalo bwana Mandela alifungwa kwa miaka
27.
Rais Obama
pia atakutana na kiongozi mwenzake wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
Mshauri
msaidizi wa usalama wa kitaifa nchini Marekani, Ben Rhodes aliiambia Sauti ya
Amerika-VOA kwamba miongoni mwa masuala ambayo bwana Obama inaonekana
atazungumzia ni suala la Zimbabwe ambayo inaelekea kufanya uchaguzi wa urais.
Rhodes
alisema Marekani inataka kuona uchaguzi huru, sawa na wenye hadhi nchini
Zimbabwe pamoja na nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari na mambo mengine ya
demokrasia nchini humo.
Marekani
inamshutumu Rais Robert Mugabe kwa kutumia ukandamizaji na wizi kushinda
uchaguzi wa urais uliopita ikiwemo ghasia na mzozo kwenye vituo vya kupiga kura
mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment