Majeruhi wa
ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani.
|
Gari
la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika
Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
|
Kichanga cha Miezi 6 kimefariki Dunia papo hapo na
wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa katika ajali mbaya iliyohusisha
Basi kampuni ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro
pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere nje kidogo ya Jiji la
Mbeya.
Kwa
mujibu wa Wahanga wa ajali hiyo iliyotokea jana (Juni 26,2013)wamesema
imetokana na mwendokasi ambapo Dereva alishindwa kulimudu basi hilo lililokuwa
likitokea mkoani Mbeya kuelekea mkoani Mwanza.
Wamesema
ajali hiyo imetokea majira ya Saa moja asubuhi ambapo katika ajali hiyo
watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya huku
wengine wakipatiwa huduma ya kwanza kisha kuendelea na safari baada ya
kubadilishiwa gari.
Gari
hilo lenye namba za usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa
kuendelea na safari ndipo lilipoletwa basi lingine la kampuni hiyo hiyo ya
Sabena kwa ajili ya kuendelea na Safari.
Kondakta
wa Basi hilo Seif Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari
uliosababisha kupasuka kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa kusimama na
kutumbukia mtaroni.
Amemtaja
Dereva wa basi hilo kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa alikimbia
baada ya ajali hiyo ingawa kondakta alitoa taarifa kuwa kafuata matibabu
Hospitalini.
Picha
na Mbeya yetu.
No comments:
Post a Comment