Umbea una faida kiafya. |
Katika jamii
yoyote mtu mwenye tabia ya umbea huchukiwa, hutengwa na hata wakati mwingine
hupigwa kwa kuonekana kuwa ni chanzo cha migogoro na huku viongozi wa dini
wakimwona mtu wa aina hiyo kuwa ni mtenda dhambi.
Watu
wanaopenda tabia ya umbea huenda wakawa wamepata mtetezi. Ripoti iliyotolewa
hivi karibuni kuhusu tabia ya watu kupenda kutumia muda mwingi kusema mambo ya
watu wengine, inasema tabia ya umbea ina manufaa kiafya.
Ripoti hiyo
iliyotolewa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Rhode Island cha Marekani,
inasema kuwa watu wanaonufaika zaidi za tabia hiyo ni wale wanaopenda kuongea
mambo mabaya wa watu wengine kuliko wenzao wanaopenda kuzungumza kuhusu mambo
mazuri.
Wataalamu
hao wamebaini kuwa iwapo mtu atatumia dakika 20 kuzungumzia mambo mabaya ya
watu wengine, anaweza kuimarisha afya yake kwa kupunguza msongo wa mawazo, woga
na mashaka kwa asilimia 96 kwa muda wa masaa manne mfululizo.
Hata hivyo,
wamebainisha kuwa mtu akitumia muda huo huo kuzungumza mambo mazuri ya watu
wengine, atapunguza msongo wa mawazo kwa asilimia 72 ikimaanisha kuwa watu
wenye kuzungumza mambo mabaya ndio wenye kunufaika zaidi.
Watafiti
hao, wakifafanua hali hiyo wameelezwa kuwa mtu anapoongea habari nzuri
zinazowahusu watu wengine huuchochea ubongo kutaka kujiunganisha na mtu
anayezungumzwa, wakati yule anayezungumza habari mbaya huwa kinyume chake.
Mtu
anayezungumza habari mbaya anatabia ya kutokuhifadhi alichokisema, bali
huendelea na mambo yake kama kawaida, wakati anayezungumza habari nzuri hukaa
nazo moyoni kwa kipindi cha muda fulani.
Mtaalamu wa
Saikolojia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Lusajo Kajula anasema
binadamu wote huongea kuhusu watu wengine, lakini umbea ni zaidi ya maongezi.
Lusajo
anasema asili ya mwanadamu ni kuzungumza japokuwa wakati mwingine hujikuta
akiishia kutoa mifano halisi ya maisha ya watu wengine na hivyo kuingia katika
mgogoro wakati mtu aliyesemwa anaposikia.
“Umbea ni
kawaida na hauzuiliki, tatizo ni yaliyomo ndani ya umbea ambayo mara nyingi
hutegemea na mawazo mtu aliyonayo. Kama ana mawazo hasi, ataongea mambo
mabaya,” anasema Kajula.
Hata hivyo,
Kajula anapingana na dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa mwanamke ndiyo
anayependa zaidi tabia ya kuzungumza mambo ya watu wengine kuliko mwanaume.
Chanzo: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment