|
Baadhi ya
Viongozi wa Vilabu 16 vya Salam vilivyoorodheshwa Radio Kwizera leo(Juni
12,2013) 2013 wakiendelea na Mkutano wao
ndani ya ukumbi wa Radio Kwizera , wilayani
Ngara mkoani Kagera.
|
| Dotto Bahemu akichukua taarifa kuhusu wale waliochaguliwa kuwa Viongozi wa Vilabu 16 vya Salam vya Radio Kwizera leo(Juni 12,2013) 2013 katika Ukumbi wa Radio Kwizera mjini Ngara mkoani Kagera. |
| Hawa ndio Viongozi waliochaguliwa na Baadhi ya Viongozi kuungoza Vilabu 16 vya Salam vya Radio Kwizera leo(Juni 12,2013) 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa Radio Kwizera mjini Ngara mkoani Kagera. |
| Baadhi ya Viongozi wa Vilabu 16 vya Salam vya Radio Kwizera wakiwa kwenye Mkutano wao Mkuu leo(Juni 12,2013) 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa Radio Kwizera mjini Ngara mkoani Kagera. |
Mkutano wa
RK Salam Club's Jun 12,2013 katika Ukumbi wa RK mjini Ngara wakiwa hapa pamoja
na Mengine wakichagua Rais wa RK Club,Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu ili kukuza Upendo,Amani,Ushirikiano na Maendeleo katika Jamii.
RK Salam
Club's hizo ni pamoja na Muungano RK
Salam Club,Nterungwe RK Salam Club,Wema
RK Salam Club,Mwilamvya RK Salam Club,Laight
RK Salam Club Lulembela,Nyakisasa RK Salam Club,Biharamulo RK Salam Club,Ushirikiano RK Salam Club,Uhuru
RK Salam Club,Umoja RK Salam Club,Wazalendo RK Salam Club.
Uchaguzi huo
wa Umoja wa Watuma Salamu wa Radio Kwizera (RK
Salam Club's) umehusu Wajumbe wake ambao ni Mwenyeviti,Katibu na
Wahasibu wa Vilabu 16 Vilivyosajiliwa na Hai vya Radio kwizera kuchagua Uongozi
wa Umoja huo kwa nafasi ya Rais ,Makamu
Rais,Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi,Mhasibu Mkuu pamoja na Kamati ya Nidhamu.
Akitangaza
motokeo Katika Uchaguzi huo ,Mwenyekiti
wa Uchaguzi Seif Omary Upupu amesema Jumla ya wapiga kura walikuwa ni 34 na kumtangaza
Rais aliyechaguliwa kuwa ni Mwl.Joshua
Kaijage kwa kupata kura 23 kutoka Mwilamvya RK salam CLub,akiwashinda wagombea
wenzake Paskari Mbugani kura 8 na Clemence Nyandindi kura 3.
Makamu wa
Rais wa Umoja wa Vilabu hivyo vya RK ni Kawese Andrea kutoka Nyakisasa RK salam
Club kwa kura 13,akiwashinda Paschal Mbugani kura 11 na Clemence Nyandindi kura
10.
Katibu Mkuu
wa Umoja huo wa Vilabu vya Salama Vya Radio Kwizera ni Yasin Gwamasunzu kutoka
RK Laight Salam Club kwa kupata Kura 22 na kuwashinda wagombea wenzake Sinani
Ngomambili kura 8,Erenest Kuguru kura 2 huku kura 2 zikiharibika.
Aidha katika
Nafasi ya Katibu Msaidizi wa umoja huo,ametangazwa ni Paschal Mbugani aka Mzee
wa Haba na Haba kutoka Wema RK Salam Club kwa kupata kura 21 na kuwashinda Juma
Ayubu aliyepata kura 8 na Melkior Sheshahu kura 4 huku kura Moja ikiharibika.
Mwenyekiti
wa Uchaguzi huo Seif Omary Upupu amemtangaza
Papa Clemence Nyandindi kuwa Mhasibu wa Umoja huo wa Salama Radio
Kwizera kwa Kupata kura 23,akiwabwaga wapinzani wake Sixmundi Mgalula kura 7 na
Kachumita Zefrini kwa kupata kura 7 huku
kura moja ikiharibika.
Katika
mkutano huo Mkuu wa Vilabu vya Watuma Salam wa Radio Kwizera,ilichaguliwa
Kamati ya nidhamu ya watu watano ambao ni pamoja na Richard Galila,Amon
Zenobi,Sixmundi Mgalulua,Bandora Kakenguzi na Marindi wa Marindi.
Ikumbukwe
kuwa Radio Kwizera iliona Umuhimu wa kuwa karibu na Vilabu
hivyo vya Salam ili kuwaleta watu pamoja, ili washirikiane kwa pamoja lengo likiwa ni kuleta Umoja,Upendo na Maendeleo katika Jamii.
Vilabu hivyo Vya Salam Vilivyosajiliwa Radio Kwizera ambavyo
ni hai ni pamoja na:-
:- Mwilamvya RK
Salam Club ,wilayani Kasulu.
:- Umoja RK
Salam Club,Mwanga Barabarani wilayni Biharamulo.
:- Light RK
Salam Club,Lulembela wilayani Bukombe.
:- Amani RK
Salam Club,Kalambi wilayani Muleba.
:- Muungano
RK Salam Club,Muzani Nyakahura wilayani Biharamulo.
:- Camp la
Waparanganaji RK Salam Club,Ushirombo.
:- Wema RK
Salam Club,Ruganzo wilayani Biharamulo.
:- Kumwendo
RK Salam Club,wilayani Ngara.
:-
Ushirikiano RK Salam Club ,Katahoka wilayani Biharamulo.
:- Nterungwe
RK Salam Club,Nterungwe wilayani Ngara.
:- Chapa
Jembe RK Salam Club,Nyabusozi wilayani Biharamulo.
:-
Biharamulo RK Salam Club,wilayani Biharamulo.
:- Wazalendo
RK Salam Club,Kazilamyaye Runzewe.
:- Mauzo
Basanza RK Salam Club,wilayani Uvinza Kigoma.
:- Kibondo
RK Salam Club, wilayani Kibondo.
:- Nyakisasa
RK Salam Club,wilayani Ngara.
Aidha Radio Kwizera FM ya Wilayani Ngara mkoani Kagera ni Mlezi wa Vikundi hivyo vya Salama na wanaunganishwa kupitia kipindi cha RK Salam Club kila siku za Jumatano na Ijumaa kwa Lengo la kukuza Amani,Upendo,Ushirikiano na Maendeleo katika Jamii wanayoishi.





No comments:
Post a Comment