Siku 13
baada ya kifo cha mwanamuziki wa kizazi
kipya, Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwair’, ripoti ya daktari inayoeleza sababu
halisi ya kifo chake bado utata mtupu kwani haijawekwa wazi, hivyo kuwafanya
wengi kuendelea kuamini uvumi.
![]() |
|
|
Kuhusu
uvumi, vitu viwili vinavyotajwa sana ni ama kifo chake kilisababishwa na
kuchanganya madawa ya kulevya pamoja na vilevi vingine, hivyo kutengeneza sumu
iliyomuua au alibeba mzigo wa unga tumboni ambao ulimchachia na kumtanguliza
mbele ya haki.
Huku
tukisubiri ripoti hiyo kuwekwa wazi, Uwazi lipo kwenye wakati mzuri kueleza
kinagaubaga jinsi wasanii wa Kitanzania walivyogeuzwa makuli wa kubeba mizigo
ya madawa ya kulevya tumboni na kusafirisha kwenda nchi mbalimbali.
Habari
zinaeleza kuwa wasanii mbalimbali nchini, wameingia kwenye mkumbo wa
kusafirisha unga tumboni kutokana tamaa ya utajiri na wakati mwingine ni baada
ya kuona maisha yao ya kimuziki hayawaendei vizuri.
Kutokana na
kuingia kwenye biashara hiyo, wasanii hao hususan wanamuziki, hutambuliwa zaidi
kwa jina maarufu la punda, kwa tafsiri kwamba wao ni sawa na mnyama huyo ambaye
kazi yake kubwa ni kubeba mizigo ya binadamu.
Hoja kuhusu
jina hilo ni kwamba wanaobeba madawa ya kulevya tumboni, wanajishusha thamani
sawa na punda, kwani binadamu ni wale matajiri wanaowabebesha mizigo hiyo.
![]() |
|
Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’.
|
USHUHUDA WA
SUGU
Ukweli wa
jinsi matajiri wauza unga wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania kama punda,
unapewa nguvu na ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema),
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Mbunge huyo
ambaye anapewa heshima kwamba ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza
mwandishi wetu kuwa kabla hajawa memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi
kufuatwa na wauza unga kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya nchi.
“Jamaa
waliniambia kwa sababu mimi nasafirisafiri sana, passport (hati ya kusafiria)
yangu itakuwa imeshagongwagongwa sana, kwa hiyo ni rahisi kwenda nchi
tofautitofauti kwa urahisi, kwa hiyo wakataka niwe nabeba unga.
“Kigezo cha
pili waliona kwa sababu mimi ni mwanamuziki, kwa hiyo ni rahisi watu kuamini
ziara zangu ni za kimuziki. Nilikataa, niliwaambia siwezi kufanya biashara hiyo
kabisa,” alisema Sugu.
Mwaka 2011,
mbunge huyo aliwahi kugusia hilo, wakati akitoa hoja kuchangia bajeti ya Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa serikali ni lazima iwasaidie
wanamuziki wa Kitanzania kwa sababu wanaibiwa sana, hivyo kuwafanya vijana
kuona kimbilio rahisi la kutajirika ni kuuza madawa ya kulevya.
“Mheshimiwa
spika, serikali isifanye ili kijana wa Kitanzania afanikiwe lazima auze unga,
madawa ya kulevya,” alisema Sugu na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa
kushawishiwa na matajiri wa unga ili naye awe punda.
![]() |
|
Jack Patrick.
|
PUNDA
HULIPWA DOLA 3000 MPAKA 5000
Kwa mujibu
wa mwanamuziki maarufu wa dansi nchini (jina tunalo), kwa wastani punda hulipwa
fedha kulingana na umaarufu wake, kwa kuangalia kiwango cha mzigo anaobeba,
vilevile nchi anayopeleka.
“Mara nyingi
watu wanalipwa dola 3000 (shilingi 4,800,000) mpaka dola 5000 (shilingi
8,000,000). Binafsi nilishabeba madawa kutoka hapa Tanzania kwenda China,
Botswana na Afrika Kusini, kila nilipofikisha mzigo nililipwa dola 5000,”
alisema mwanamuziki huyo na kuongeza:
“Kuna
kipindi nilinogewa, nikawa sijishughulishi sana na muziki, kila mara nipo
safarini nakwenda kupeleka mzigo, nikirudi nipo vizuri na dola 5000 zangu. Hivi
sasa nimeacha baada ya watu wangu wa karibu kunishauri na kunieleza kwa mapana
hatari inayoweza kunipata.”
MTINDO WA
SASA
Utafiti wa
siku za hivi karibuni, umepata jawabu kwamba wauza unga wengi, wanawatumia
wanamuziki na wasanii mbalimbali kusafirisha mizigo kwa sababu kwao ni rahisi
kugongewa visa katika balozi za nchi wanazokusudia kwenda.
“Kule
inaweza kuandaliwa shoo ya uongo na kweli, wewe unasafiri kwamba unakwenda
kwenye hiyo shoo lakini kumbe ni utapeli mtupu. Kule hauendi kama mwanamuziki,
isipokuwa ni punda tu,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Fikiria mtu
unakwenda kwenye shoo halafu ukumbini wanaingia watu 40, halafu huyo mwandaaji
anakulipa fedha zako vizuri, unalala hoteli nzuri, ukumbi analipa, kodi anatoa.
Hii biashara ya madawa ya kulevya ina siri kubwa.
![]() |
|
Khaleed Mohamed ‘TID’.
|
“Kinachosikitisha
kwa wanamuziki wenzetu ni kwamba hawajitambui. Watu wanakufa jamani, kukubali
kusafirisha madawa tumboni ni sawa kujiweka katikati ya uhai na kifo. Zile dawa
zikipata joto tumboni huponi. Ukijisahau na kunywa kitu cha moto ni kifo.”
Mtoa habari
huyo aliendelea kubainisha kuwa wanamuziki wa Kitanzania wengi wanakuwa nchini
bila kazi mpaka wanakumbwa na hali ngumu ya uchumi kutokana na kutopata shoo za
kutosha, hivyo kuwawia rahisi kukubali ofa ya kubeba madawa ya kulevya tumboni
kwenda nchi mbalimbali.
“Hivi sasa
kuna wimbi kubwa. Watakwenda hivyo ila baadaye madawa hufeli tu. Naamini
itafika wakati tutashuhudia vifo vingi vya wanamuziki wetu. Mungu akiniweka hai
nitasema, kwani nawajua wanamuziki wengi punda,” alisema.
Aidha, mtoa
habari huyo aliwataja wanamuziki sita nchini ambao aliwataja moja kwa moja kuwa
wanajishughulisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya lakini majina yao
tunayahifadhi kwa sasa.
![]() |
|
Ambwene Yesayah ‘AY’.
|
MWANAMUZIKI
ALIVYOMSHAWISHI MFANYABIASHARA
Kuna
mwanamuziki (jina kapuni) ambaye hivi karibuni alirejea nchini baada ya kupata
matatizo akiwa nje ya nchi, aliwahi kumshawishi mfanyabiashara mmoja aingie
kwenye biashara ya madawa ya kulevya halafu yeye atakuwa anabeba.
Mfanyabiashara
huyo (naye jina kapuni), alisema: “Nilishangaa yule dogo ananiambia yeye yupo
tayari kubeba mzigo kusafirisha kwenda Afrika Kusini na nchi nyingine za Kusini
ya Afrika.
“Aliniambia
yeye ameshaweza kubeba madawa ya wafanyabiashara wengine na wakapata faida
kubwa. Aliniambia faida ni mara mbili kwa asilimia 100. Nilimjibu siwezi
kufanya hiyo biashara, baadaye akiwa huko alipata matatizo na hivi sasa yupo
hapa nchini.”
MAMA WA
MWANAMUZIKI NI TISHIO KWA KUUZA UNGA
Mama wa
mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva (jina tunalo), mkazi wa Magomeni, Dar es
Salaam, ni tishio kwa biashara ya kuuza unga.
Kwa mujibu
wa vyanzo vyetu, mama huyo amekuwa akiwatumia mabinti mbalimbali wa Jiji la Dar
es Salaam, kuwabebesha mizigo tumboni na kuwasafirisha kwenda China na nchi za
Kiarabu ambako ndiko lilipo soko lake.
“Wapo
watangazaji wameshabebeshwa mizigo na yule mama. Yeye hasafiri na mzigo na ana
watoto lakini hawabebeshi mizigo watoto wake, ila anawatumia watoto wa
wenzake,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Kama
ingekuwa ni biashara nzuri kwa nini yeye habebi wala watoto wake? Hawa dada
zetu ambao wanapenda sana maisha ya haraka, inabidi wawe macho, vinginevyo
watakwenda na maji.”
|
Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.
|
UPO MFANO WA
BINTI KIZIWI
Mrembo
Sandra Khan, aliyepata jina la Binti Kiziwi baada ya kushiriki video ya wimbo
wa Binti Kiziwi ambao ni mali ya mwanamuziki Ally Mohamed Ahmad ‘Z-Anto’,
alikamatwa Februari, mwaka huu China na kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya
tumboni.
Zipo tuhuma
kwamba Binti Kiziwi, alikuwa kwenye safari moja na mwanamitindo Jacqueline
Patrick ambaye aliingia mitini baada ya kumwona mrembo huyo ambaye ni mtalaka
wa Z-Anto, akikamatwa na polisi wa China.
Madai
yanasema kuwa Binti Kiziwi aliishiwa nguvu na kupata maumivu makali ya tumbo
baada ya kuwasili China, hivyo polisi walimchukua kwa lengo la kumpa huduma ya
kwanza ndipo wakabaini kwamba alikuwa amebeba madawa ya kulevya tumboni.
Jack Patrick
anakiri kwamba alishuhudia Binti Kiziwi akikamatwa, ila aliona soo kujitokeza
kusema anamjua, kwani naye angewekwa ndani kama mtuhumiwa.
Upande
mwingine, mume wa Jack Patrick, Abdulatif Fundikira, hana muda mrefu tangu
aachiwe kwa dhamana, akikabiliwa na kesi ya usafirishaji wa madawa ya kulevya.
![]() |
| ‘MwanaFA’, |
WANAMUZIKI
WANAVYOONGEA
Mwana-Hip
Hop, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, alisema kuwa yeye hajawahi kusafirisha madawa ya
kulevya tumboni, kwani anafahamu kuwa kufanya hivyo ni tatizo, alifafanua:
“Ndiyo maana
mimi nafanya muziki kuelimisha jamii, kwa hiyo siwezi kufanya biashara ya
madawa ya kulevya. Watu wanaingia kwenye hiyo biashara ili watajirike mapema,
hicho ni kitu kibaya sana. Nawaomba wale wanaouza madawa ya kulevya wabadilike,
jamii inawategemea.”
Mkali wa
Bongo Fleva, Ambwene Yesayah ‘AY’ alisema: “Mimi sijawahi kuthibitisha kama
kweli wanamuziki wenzetu wanafanya hivyo, ila kama kweli wanafanya basi
wanahatarisha maisha yao. Kila anayefanya hivyo ajue kwamba akikamatwa ndiyo
mwisho wake. Nashauri wanamuziki tusipende maisha ya mkato.”
Seif Shaaban
‘Matonya’, alisema: “Mimi nimeshawahi kusingiziwa kwamba nilikamatwa nje ya
nchi kitu ambacho siyo kweli. Kwa watu ambao wanafanya hiyo biashara,
nawashauri waache, kwani madawa ya kulevya yanatuharibia ndugu zetu.”
Mwanamuziki
wa mduara, Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole’ alisema: “Mimi sijawahi kuona, ila
kama ni hivyo waachane na hiyo biashara kabisa.”
ATHARI ZA MADAWA KULEVYA
Wapo
wanamuziki mbalimbali ambao wameshatajwa kwamba wanajihusisha na matumizi ya
madawa ya kulevya, wimbi limekuwa kubwa mno.
Mwana-Hip
Hop, Kulwa Maujanja wa Kundi la Mapacha, aliwahi kutoa ushuhuda wake kwa
mwandishi wetu kwamba aligongea sigara kwa wanamuziki wenzake wawili (majina
tunayo) na alipovuta, alikuta imewekewa madawa ya kulevya.
“Kichwa
kiliamka nikawa kama nimedata. Kesho yake nilishinda kichwa kinauma sana. Kumbe
wale ndugu zetu wanatumia madawa ya kulevya, wanachanganya kwenye sigara,”
alisema Kulwa.
Rashid
Makwilo ‘Chid Beenz’, aliwahi kukaririwa kwamba ameacha madawa ya kulevya kama
ilivyo kwa mwana Hip Hop mwenzake, Langa Kileo, ingawa yapo madai kuwa wawili
hao bado hawajaacha.
Wanamuziki
wengine, Khaleed Mohamed ‘TID’, Msafiri Saidi ‘Diouf’, Aisha Mbegu ‘Madinda’ na
wengine kibao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na utumiaji wa mihadarati.
Kuhusu
athari zake, inashauriwa kitaalamu kwamba ni vema kuacha kutumia madawa, kwani
huharibu ubongo kwa sababu huua mishipa ya fahamu, huathiri mfumo wa damu,
husababisha mhemko na juu ya yote ni huchochea shambulio la moyo (cardiac
arrest) na vifo vya ghafla.
![]() |
|
Albert Mangweha.
|
NGWAIR NA M2
THE P
Kuhusu
Ngwair, alikuwa na rafiki yake Mugaza Pembe ‘M2 The P’, wote walizidiwa pamoja
lakini yeye alifariki dunia na kumwacha mwenzake akiwa mahututi kwenye
Hospitali ya Mtakatifu Helen Joseph, Johannesburg, Afrika Kusini.
Yapo mambo
matatu ambayo yanadaiwa lakini ripoti ya daktari au kauli ya M2 The P, ndivyo
vinavyoweza kumaliza utata.
Mambo hayo
matatu ni kwamba walizidisha kiasi cha unga, madai mengine ni kwamba walitumia
madawa yaliyoisha muda wake, hivyo kuwa sumu, tatu ni kuwa walikuwa na mzigo
tumboni ambao ulifumuka.
Chanzo: GLOBAL













No comments:
Post a Comment