![]() |
| Rais wa Rwanda Paul Kagame. |
Rais Kagame alimtukana Rais Kiwete kwa kuita ushauri
wake kwamba ni ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa, awali Rais Kikwete
alizishauri nchi za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa
njia ya amani.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa
kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao
Makuu ya AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni
vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo
DRC Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.
“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi
nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa
na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais Kagame.
Katika hatua nyingine Rai Kagame alisema kwamba
ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea wanyarandwa mbele ya
mataifa. Rais Kagame aliyasema hayo katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya
maofisa wa jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo ya kijeshi siku ya Juma
Tatu nchini Rwanda.
Ingawa haijajulikana mara moja kwamba baadhi ya watu
walioandika maoni yao katika mtandao wa Facebook ni watanzania ama baadhi yao
si watanzania, huku wakidai kwamba Rais Kagame yuko sahihi.
Chanzo:mwaikenda.blogspot.com






No comments:
Post a Comment