Msanii wa Bongo Fleva Langa Kileo Afariki dunia ....R.I.P.....Jembe.... (Dec 22, 1985-Jun 13, 2013). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 13, 2013

Msanii wa Bongo Fleva Langa Kileo Afariki dunia ....R.I.P.....Jembe.... (Dec 22, 1985-Jun 13, 2013).




Langa Kileo enzi za uhai wake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Langa Mengisen Kileo, leo jioni amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar baada ya kuugua malaria na kisha kujitokeza homa ya uti wa mgongo.




Akizungumza na waandishi wa Habari, Baba mzazi wa Langa, Mzee Mengesen Kileo  amesema alimpeleka mwanaye Hospitali ya Kinondoni maarufu ‘Kwa Dokta Mvungi’ ambapo aligundulika kuwa na malaria na baadaye aligundulika kuwa na homa ya uti wa mgongo. 




Mzee Mengisen aliongeza kuwa, baada ya Dokta Mvungi kugundua kuwa Langa ana homa ya uti wa mgongo ambayo ni hatari, leo(Juni 13,2013)  asubuhi aliamua kumkimbiza hospitali ya Muhimbili na kumfikishia chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’. 




Baba huyo wa marehemu alizidi kuueleza kuwa, ilipofika mida ya saa kumi jioni, mwanaye aliaga dunia. 




Mipango ya mazishi inaendelea kupangwa nyumbani kwao marehemu Mtaa wa Chato, Mikochocheni jijini Dar. 





Langa Kileo enzi za uhai wake.
Langa alizaliwa Desemba 22, 1985 jijini Dar es Salaam katika familia ya wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.




Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam. 




Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. 




Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma. 




Langa alitamba kwa nyimbo zake kama Pipi ya Kijiti, Matawi ya Juu, Gangsta na Rafiki wa Kweli aliyoiachia juzi Jumatatu.




Langa alikuwa ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha akiwa pamoja na Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwijage `Witness’ ambapo walitamba na nyimbo kama Unaniacha Hoi na Kiswanglish.




Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad